Serikali
inakamilisha taratibu zakupata mkopo toka serikali ya China bilioni 500
kwaajili ya ujenzi wa nyumba 3500 za askari wa jeshi la polisi nchini
kufikia mwaka 2025.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Masauni Yusufu Masauni ameyasema
hayo leo mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Tunduma
Mheshimiwa Frank Mwakajoka aliyetaka ufafanuzi wa lini serikali
itaboresha na kuongeza nyumba za askari polisi nchini.
Naibu
Waziri Masauni amesema kuwa ni dhamira ya serikali kuhakikisha jeshi la
polisi linaboresha makazi na kuwa na ofisi ili kuwezesha utoaji wa
huduma kwa wananchi kuwa mzuri na pindi mkopo huo utakapo kamilika
ujenzi utaanza kwa Tanzania Bara na Zanzibar.
Naibu
Waziri huyo ameongeza kuwa kwa sasa wapo katika mpango wa awali wa
kujenga nyumba 350 nchi nzima ambazo zitatatua tatizo hilo la walinzi wa
raia na mali za wa Tanzania kukosa makazi bora na ya kudumu.
No comments:
Post a Comment