Alikuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba na Mwanaharakati, Humphrey Polepole, amesema CCM ndiyo chama pekee cha siasa nchini chenye misingi ya kuwatumikia wananchi ukilinganisha na vyama vingine vya siasa.
Alisema Jimbo la Iringa Mjini halikupaswa kwenda upinzani hivyo aliwataka viongozi wa CCM mkoani humo kujitathimini na kuona wapi walipoanguka ili waweze kulirudisha mwaka 2020.
Polepole aliyasema hayo jana wakati akifungua Kongamano la Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu la CCM mkoani humo.
Aliongeza kuwa, utendaji mzuri wa Serikali ya Rais Dkt. John Magufuli katika kutekeleza Ilani ya CCM, umedhihirisha wazi aina ya wana CCM ambao ni hazina wanaoweza kuleta maendeleo makubwa kwa jamii na nchi kwa ujumla.
Aliwataka wana CCM mkoani humo, kuanza kueleza mambo mazuri yanayofanywa na Rais Dkt. Magufuli katika utekelezaji wa Ilani ya CCM.
Polepole alisema kinachofanywa na Rais Dkt.Magufuli juu ya kuwatumikia Watanzania, kimewafanya wananchi watambue hazina kubwa iliyopo ndani ya CCM.
"Katika Uchaguzi Mkuu 2015, CCM ilipata ushindi wa asilimia 58 ambao si mzuri sana tunaoweza kujivunia...nguvu iongezwe zaidi ili tupate ushindi wa asilimia 80 hadi 88.
"Njia pekee ya kuongeza ushindi wa CCM, lazima tufanye kazi ya kukijenga chama," alisema Polepole
No comments:
Post a Comment