Rais
Dk. John Magufuli ameidhinisha kuwepo kwa wilaya tano katika jiji la
Dar es Salaam, badala ya tatu zilizokuwepo awali, ili kuleta maendeleo
ya haraka hususan katika elimu.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki, alisema juzi kuwa, waliwasilisha
ombi la ugawaji wa wilaya za Kinondoni na Temeke kwa rais, ambapo
ameshaliidhinisha.
“Hatua
hii ya kuwepo kwa wilaya tano italiwezesha jiji la Dar es Salaam,
kupata maendeleo ya haraka kwa kugawanywa kwa wilaya hizo, ambapo
kutakuwa na usimamizi thabiti na hakutakuwa na kisingizio cha kuelemewa
kwa majukumu kwa watendaji,”alisema.
Aliomba katika ugawaji wa wilaya hizo, rasilimali zilizopo na mipaka igawanywe kwa manufaa ya wananchi wa wilaya hizo.
Aidha,
alisema kinachosubiriwa ni ugawaji wa mipaka na kutangazwa rasmi
kuongezeka wilaya mbili ya Kigamboni na Ubungo na kufikisha idadi ya
wilaya tano katika jiji la Dar es Salaam.
Akizungumzia
ombi la ugawaji wa wilaya za Kinondoni na Temeke, Sadiki alisema hadi
kufikia juzi, ombi hilo lilishaidhinishwa na rais, hivyo Kinondoni
itakuwa na wilaya mbili za Kinondoni na Ubungo huku wilaya ya Temeke
ikiwa na wilaya za Temeke na Kigamboni
No comments:
Post a Comment