Jaji
mkuu wa Tanzania Mh. Mohamed Othman Chande amesema idara ya mahakama
ipo katika mchakato wa kuangalia upya masharti ya dhamana yanayotolewa
katika mahakama za mwanzo baada ya kubainika kuwa ni magumu hali
inayochangia mlrundikano wa mahabusu katika magereza yote nchini.
Jaji
Chande aliyasema hayo jana jijini Dar es salaam katika uzinduzi wa wiki
ya elimu ya sheria nchini katika viwanja vya Mnazi Mmoja ambapo alisema
sharti la dhamana sio adhabu kwa mtuhumiwa na kusisitiza kuwa tayari
mahakimu katika ngazi za Mahakama za Mwanzo, Wilaya na mikoa wameanza
kutafuta njia ya kupunguza idadi ya mahabusu.
Aidha
katika uzinduzi huo idara ya mahakama imesema inaangalia uwezekano wa
kutoa adhabu mbadala kwa wafungwa waliohukumiwa kifungo cha chini ya
miaka mitatu ikiwemo vifungo vya nje kwa kufanya kazi za kijamii
zinazosimamiwa na idara ya ustawi wa jamii.
No comments:
Post a Comment