Wafanyabiashara
wanne wa Tanzania wameuwa kwa kupigwa risasi kisha kuchomwa kwa vitu
vyenye ncha kali nchini Msumbiji baada ya kuvamiwa na watu wanaosadikiwa
kuwa ni majambazi.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Henry Mwaibambe alisema tukio hilo lilitokea
usiku wa Jumatatu iliyopita katika machimbo ya dhahabu, Kijiji cha Mtoro
Mtupweshi Kamprigando.
Aliwataja
waliofariki dunia kuwa ni Salum Mfanga (44) Mkazi wa Temeke, Dar es
Salaam, Yusuph Twalibu (34) na Mariam Ramadhani (30) wakazi wa Tanga na
Hamisi Mkapira (40) wa Morogoro.
Kamanda
huyo alisema kifo cha Mariam ambaye alifanikiwa kujiokoa,
kilisababishwa na kukosa huduma ya haraka baada ya kuvunjika mguu.
Kamanda
huyo alisema wafanyabiashara hao walivamiwa na majambazi waliokuwa na
risasi pamoja na mapanga katika vibanda vya kubadilishia fedha nchini
humo. “Miili ya wafanyabiashara hao ililetwa na ndugu zao ambao wanaishi Msumbiji,” alisema.
Wakizungumzia
tukio hilo, Said Mfanga na Dotto Ramadhani ambao ni ndugu wa marehemu
hao walisema baada ya kuwaua, majambazi hao waliwapora fedha pamoja na
mabegi yao.
No comments:
Post a Comment