Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) imeikabidhi Kampuni ya Udalali ya Yono
kuwafilisi wateja 24 wanaodaiwa kodi ya Sh bilioni 18.95 baada ya
kutorosha makontena ya mizigo yao kwenye Bandari Kavu (ICD) ya Azam
mwishoni mwa mwaka jana.
Majina
ya wadaiwa hayo yametolewa jana kwenye vyombo mbalimbali vya habari, na
Kampuni hiyo ya Udalali ya Yono baada ya TRA kuwakabidhi kazi ya
kuwafilisi kutokana na kushindwa kutekeleza wajibu wao baada ya kupewa
muda wa kulipa kodi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni hiyo, Yono Kevela jana alisema wamepewa amri na TRA
ya kisheria ya kukamata mali za wadaiwa na kuwafilisi ili kulipia kodi
wanazodaiwa.
Kevela
alisema baada ya kupata kazi hiyo, wao wameona busara kuwatangaza
kwenye vyombo vya habari na kuwapa siku 14 kulipa kodi wanazodaiwa na
kwamba baada ya muda huo kumalizika, hatua za kukamata mali za wadaiwa
hao zitaanza na kuwafilisi.
“Tumekabidhiwa
wadaiwa 24 na TRA, hawa wamekwepa kodi kwa kutorosha kontena katika
Bandari Kavu ya Azam mwishoni mwa mwaka jana, sasa walipewa muda wa
kulipa ila wamekaidi, sasa kazi tumepewa sisi na tutawafilisi mali zao
zote ili kulipa deni hilo,” alifafanua Kevela.
==>Majina ya wadaiwa hai na kiasi cha fedha wanachodaiwa kwenye mabano ni
- Zulea Abas Ali (16,760577.24)
- Omary Hussein Badawy (21,346,615.40)
- Libas Fashion (26,593,245.78)
- Said Ahmed Said (28,249,352.50)
- Strauss International (45,393,769.95)
- Farid Abdallah Salum (52,185, 614.97)
- Ally Awes Hamdani (55,485,904.07)
- Nasir Saleh Mazrui (60,105,873.77)
- Simbo Yona Kimaro (64,221,009.10)
- Zuleha Abbas Alli (75,508,551.88)
- Issa Ali Salim (94,543,161.96)
- Ally Masoud Dama (102,586,719.22)
- Juma Kassem Abdul (130,182,395.12)
- Salum Link Tyres (233,447,913.31)
- Tybat Trading Co. Ltd (448,690,271.90)
- IPS Roofing Co. Ltd (966,723,692.10)
- Tifo Global Trading Co Ltd (1,573,300,644.58)
- Lotai Steel Tanzania Ltd (5,476,475,738.19)
- Tuff Tyres General Co Ltd (7,435,254,537.03)
- Swalehe Mohamed Swalehe (34,687,165.00)
- Rushwheel Tyre General Co Ltd, (1,802,988,679.20)
- Said Ahmad Hamdan (68,362,558.31)
- Ahmed Saleh Tawred (59,237,578.40)
- Farida Abdullah Salem (75,334,871. 85).
Kevela
alisema wadaiwa hao wanapaswa kulipa madeni yao ndani ya siku 14
walizopewa na kwamba iwapo watashindwa kutekeleza amri hiyo, kampuni
hiyo itaanza kazi ya kukamata mali zao na kuwafilisi.
Alisema
ili kurahisisha kazi hiyo, Kampuni ya Said Salum Bakhresa (SSB) ambayo
ndiyo mmiliki wa Bandari Kavu ya Azam pamoja na Kampuni ya Regional
Cargo Services wanapaswa kutoa ushirikiano kuhakikisha wadaiwa hao
wanalipa kodi walizokwepa.
“Kampuni
hizo zinahusishwa na kutoroshwa kwa kontena 329 zilizokuwa Azam ICD,
sasa ni vyema watoe ushirikiano ili wadaiwa walipe fedha za serikali,” alifafanua Kevela.
Alisema
baada ya muda waliotoa kumalizika, wahusika watapaswa kulipa na gharama
za ziada ambazo ni pamoja na faini na usumbufu wa kuwatafuta.
Desemba
12, mwaka jana, aliyekuwa Kaimu Kamishna wa TRA, Dk Philip Mpango
aliwaambia waandishi wa habari kuwa kampuni 15 kati ya 43 zilizokwepa
kodi baada ya kutorosha kontena 329 katika ICD ya Azam, zimelipa.
Dk
Mpango alisema Desemba 12, mwaka jana ndiyo ilikuwa siku ya mwisho
aliyotoa Rais John Magufuli ya siku saba kwa wakwepa kodi hao 43 kulipa
wenyewe kwa hiari, vinginevyo sheria zitachukua mkondo wake.
Kutokana na kauli hiyo ya Rais Magufuli, wadaiwa 15 walijitokeza na kulipa na waliobaki hawakujitokeza kulipa.
No comments:
Post a Comment