Kesi Ya Kamanda Godfrey Nzowa Dhidi Ya Kamanda Suleiman Kova Kuunguruma Leo - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Wednesday, 10 February 2016

Kesi Ya Kamanda Godfrey Nzowa Dhidi Ya Kamanda Suleiman Kova Kuunguruma LeoKesi ya maofisa wawili waandamizi wa polisi kutaka kuuziwa nyumba ya Serikali inaanza kunguruma leo katika kikao cha Mahakama ya Rufaa mjini Arusha.

Wanaopambana katika kesi hiyo ni Mkuu wa Kikosi cha Kupambana na Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa anayemshtaki kamanda mstaafu wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova.

Mwenyekiti wa Jopo la Majaji wa Mahakama ya Rufaa waliopo Arusha, Jaji Mbarouk Salum Mbarouk alisema juzi kuwa jumla ya kesi 50 zitaanza kusikilizwa wiki hii.

Alisema kati ya kesi zitakazosikilizwa, tisa ni za madai, 18 za jinai na 23 za maombi ya madai.

Mbali na Jaji Mabrouk, wengine wanaotarajiwa kusikiliza kesi hizo ni Jaji Musa Kipenka na Jaji Bernard Luanda.
Post a Comment