Shirika la kijasusi nchini Marekani FBI, miezi miwili baada ya watu kumi na wanne kuuwawa mjini Califonia na wanandoa wa kiislamu wenye itikadi kali, wachunguzi hawajabaini ushahidi wowote katika simu iliyopatika kutoka kwa mmoja wa wauaji.
Mkurugenzi wa shirirka hilo la kijasusi,James Comey amekuwa akitoa ushaidi katika kamati ya upelelezi ya seneti ya Marekani,kufuatia kupigwa kwa risasi kwa wingi San Bernardino mwezi desemba.
Bwana Comey anasema kuwa mawasiliano yao yalikuwa ni ya siri na waliweza kutumia tekinolojia ya hali ya juu kuvuruga mitambo, hivyo kuathiri sheria kuweza kuchukua mkondo wake.
Sheria ya kuondoa ulinzi wa mawasiliano hayo bado unajadiliwa mjini Washngton ili kukabiliana na mashambulizi yaliyotokea California.
No comments:
Post a Comment