Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest
Rwegasira (kulia aliyevaa kiraia) akiingia ndani ya Kiwanda cha Viatu
Gereza Karanga mjini Moshi. Rwegasira amefanya ziara kwa kukitembelea
kiwanda hicho kwa lengo la kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na
Jeshi la Magereza. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest
Rwegasira (kushoto) akimsalimia Mkuu wa Magereza mkoani Kilimanjaro,
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Venant Kayombo wakati Kiongozi
huyo wa Wizara alipowasili katika ofisi za Magereza Mkoa, mjini Moshi.
Fundi
wa Kiwanda cha Viatu Gereza Karanga mjini Moshi, Hashim Rashid
akimuonyesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja
Jenerali Projest Rwegasira (kushoto) jinsi buti la Jeshi
linavyotengenezwa ndani ya kiwanda hicho.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest
Rwegasira akiangalia buti la Jeshi lililotengenezwa na Kiwanda cha Viatu
Gereza Karanga, mjini Moshi. Kiwanda hicho kinatengenezwa viatu vya
aina mbalimbali. Kushoto ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kilimanjaro,
Venance Kayombo.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest
Rwegasira akizungumza na Maafisa wa Magereza, Polisi, Jeshi la Zimamoto
na Uokoaji na Uhamiaji mara baada ya kumaliza kukitembelea Kiwanda cha
Viatu Gereza Karanga, mjini Moshi. Rwegasira alikipongeza kiwanda hicho
na kulitaka Jeshi la Magereza kuongeza juhudi zaidi katika uzalishaji wa
viatu.
Mkuu
wa Kiwanda cha Viatu Gereza Karanga Moshi, mkoani Kilimanjaro, Kamishna
Msaidizi wa Jeshi la Magereza, Anderson James akimpa zawadi ya viatu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest
Rwegasira (kulia) mara baada ya kufanya ziara ya kukikagua kiwanda hicho
pamoja na kujifunza jinsi ya utengenezaji wa viatu unavyofanyika.
Kushoto ni Mkuu wa Magereza mkoani Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi
Mwandamizi wa Magereza, Venant Kayombo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment