Naibu
Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla akitoa hutuba fupi wakati wa tukio hilo
la kambi maalum ya matibabu ya bure kwa wananchi wote iliyoandaliwa na
Care Foundation kwa kushirikiana na wadau wengine akiwemo Mbunge wa
jimbo la Ilala, Mh. Mussa Hazan Zungu.
Naibu Waziri wa Afya, Maendejana
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla amehimiza
Jamii kuwa na utaratibu wa kupima afya mara kwa mara katika hali ya
kubaini matatizo yanayowakabili ilikuchukua hatua ikiwemo kupata tiba
mapema
Dk.
Kigwangalla ametoa kauli hiyo mapema jana Februari 28.2016, jijini Dar
es Salaam, wakati alipokuwa mgeni rasmi katika kambi maalum ya kupima
afya bure kwa wananchi mbalimbali wakiwemo wa Jimbo la Ilala kwa
kuandaliwa na Care Foundation na wadau wengine wa afya ikiwemo Hospitali
ya Ebrahim Haji Chartable Health Centre ambao wanasimamia kutoa huduma
za matibabu kwa kushirikiana na taasisi zingine.
Akitoa
hutuba yake fupi, kwa wananchi mbalimbali walifika katika tukio hilo la
kupatiwa matibabu hayo ya bure, Naibu Waziri, Dk. Kigwangalla amesema
Jamii wanatakiwa kuwa na maisha yenye afya hivyo zoezi la kupima afya
mara kwa mara ni bora zaidi kaika kuimalisha afya ya mwili.
“Wananchi
wapo na wakati mwingi wakifanya shughuli zingine na hata muda kupima
afya inakuwa ngumu. Kukinga ni bora Zaidi kuliko tiba. Zoezi hili
litasaidia sana wananchi wengi na tunaomba muendelee na maeneo yote ya
nchi yetu.” Ameeleza Dk.Kigwangalla.
Aidha,
Dk. Kigwangalla amempongeza Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Hazan Zungu
kwa kuwezesha kuandaa zoezi hilo kwa kushirikiana na wadau hao kwani ni
mfano bora wa kuigwa na wabunge wengine pindi wapatapo nafasi ya
kutumikia jamii iliyowachagua.
Pia
katika zoezi hilo, Mbune wa jimbo la Ilala, Mh. Mussa Zungu na Naibu
Waziri Dk. Kigwangalla walipata wasaha wa kupima afya zao pamoja na
kutembelea maeneo ya kutolea huduma na kushuhudia namna huduma
zinavyotolewa kwa wananchi.
Kambi
hiyo ya matibabu, inatoa matibabu hayo bure kwa wananchi wote wanaofika
hapo ambapo pia mbali na matibabu wanatoa huduma ya dawa huku wakitoa
pia mawani kwa watu wenye matatizo ya macho. Watu mbalimbali
wamekaribishwa kupatiwa matibabu hayo ambayo pia yanatolewa na madaktari
bingwa wa magonjwa husika.
Tukio likiendelea
Naibu
Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla akiwa katika meza ya kupima afya ya
mwili ikiwemo magonjwa yasio ambukiza kama vile Magonjwa ya moyo,
sukari, shinikizo la damu na mengine mengi katika zoezi linaliendelea
katika viwanja vya Bustani ya jiji iliyopo mkabara na Ukumbi wa
Karimjee.
Naibu Waziri wa Afya. Dk.Kigwangalla akiwa katika vipumo hivyo..
Mbunge wa Ilala, Mh. Mussa Hazani Zungu, akipima afya katika zoezi hilo..
Dk.
Efrahim Mika Zaky wa Msimbazi Eyes Vision Center, (kushoto) akimpima
macho mmoja wa wananchi waliojitokeza katika zoezi hilo linaloendelea
jana jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Bustani ya jiji, mkabara na
Ukumbi wa Karimjee.
Uchunguzi wa macho ukiendelea..
Dk. Efrahim Mika Zaky wa masuala ya macho, akimpima macho Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla wakati wa zoezi hilo..
Naibu
Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla akiwa katika kupima macho kwenye kambi
maalum ya kutoa huduma za matibabu ya bure yaliyoandaliwa na Care
Foundation na wadau wengine katika viwanja vya Bustani ya Jiji, Posta
Jijini Dar es Salaam.
Naibu
Waziri Dk.Kigwangalla akiwa katika moja ya sehemu ya kutolea dawa na
miwani kwa watu watakaobainika kuwa na matatizo katika macho..
Naibu
Waziri akipokea ua maalum kama ishara ya kukaribishwa katika ufunguzi
huo wa kambi maalum ya matibabu ya bure yaliyoandaliwa na CARE
Foundation na wadau wengine akiwemo Mbunge wa jimbo la Ilala, Mussa
Hazzan Zungu.
No comments:
Post a Comment