Na. Mwandishi Wetu, Liwale
Chama
cha waendesha bodaboda wilayani Liwale Mkoani Lindi chatoa mikopo ya
pikipiki kwa wanachama wake wapatao 62 zenye thamani ya shilingi
92,000,000.
Chama
hicho kilipata mkopo wa pikipiki 20 zenye thamani ya shilingi
35,000.000/= kutoka mfuko wa Maendeleo ya Vijana wa Wilaya na kuweza
kukopeshwa kwa mwanachama mmoja mmoja na kupitia umoja wao chama
kiliweza kupata pikipiki 42 na kuweza kufikia ya jumla ya pikipiki 62.
Leo
wamekabidhi pikipiki mbili kwa wanachama wawili zenye thamani ya
shilingi 4,400,000/= na kukabidhi kwa mwanachama mmoja bati zenye
thamani ya shilingi 2,000,00/= jumla ni 6,400,000/= na wameweza kufanya
marejesho ya shilingi 6,325,000/=.
Chama
hicho Kina miaka Sita Tangu kuanzishwa kwake Mnamo mwezi Mei mwaka
2010 kikiwa na waanzilishi 65 pia chama hicho kinatambuliwa na Idara ya
Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Liwale na kimepatiwa Hati ya Utambulisho
Mwaka 2014.
Mgeni rasmi bwana Wilson Nyamanga aliyekuja kumwakilisha mkuu wa wilaya ya Liwale mh,Ephraim Mmbaga.
Mgeni rasmi akikabidhi pikipiki kwa mwanacha hii leo maeneo ya ofisi za chama cha bodaboda.
Katibu wa chama cha bodaboda wilayani Liwale akisoma risara kwa mgeni rasmi.
Afisa maendeleo ya jamii wilayani Liwale bibi Mary Ding'ohi akifafanua jambo.
Kwa
sasa chama kina jumla ya wanachama 300 wenye sifa na vigezo
vinavyokidhi mahitaji ya katiba na vigezo vinavyotumika kumkopesha
mwanachama ni awe mwanachama hai na awe na kiwango cha hisa cha
mwanachama.
Pamoja
na mafanikio hayo yaliyopatikana zipo changamoto zinazowakwamisha
kushindwa kutekeleza malengo yao, changamoto hizo ni pamoja na ukosefu
wa fedha za kuendesha ujenzi wa ofisi pamoja na uwepo wa mtaji mdogo
ambao unakosesha kuwakopesha pikipiki wanachama wengi kwa wakti mmoja.
Akikabidhi
pikipiki hizo mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa wilaya bwana Wilsoni
Nyamanga ambaye ni katibu tawala wa wilaya ya Liwale amewataka waendesha
pikipiki hao kuwa na umoja kwani katika umoja huo kutasaidia kutatua
changamoto mbalimbali.
“Katika
umoja wenu imekuwa ni chanzo cha ajira na tunatambua wengi wenu
mumeepuka kujihusisha na vitendo viovyu vya kunyang’anya na kukaba pia
sisi kama watu wa ulinzi na usalama kwetu ni faraja na kama serikali
tumewatambua kama wadau wa maendeleo” alisema Nyamanga.
Hata hivyo katibu tawala huyo amewasisitizia kuzingatia sheria na
taratibu walizojiwekea katika katiba yao na kufanya maamuzi yanayoendana
na malengo yao kwa kutaka kuwepo kwa viongozi bora na wa demokrasia
ambayo mambo yote yanayofanyika yanakuwa ya wazi na shirikishi kwa
kupeana taarifa mbalimbali na kuweza kuweka malengo makubwa na kuweka
malengo yanayotekelezwa kwa kikomo.
Mmoja wa wanachama waliokabidhiwa pikipiki hizo leo Rajabu Kyula
alisema amejisikia furaha sana kukabidhiwa pikpiki kwani mwanzoni
alikuwa na pikipiki ya Bosi na sasa imekuwa mwokozi kwani sasa malengo
yake yatakuwa yametimia na ataweza kukuza kipato chake pia amewashauri
watu wengine kuweza kujiunga na chama hicho waweze kunufaika na mpango
huo wa kukopeshana pikipiki.
Pia Idi Rashidi alisema amejiskia vizuri kukabidhiwa pikipiki na
amewashauri watu wengine kujiunga na chama cha bodaboda kwani chama
hicho kimekuwa mkombozi wa vijana wengi hapa wilayani.
Mwenyekiti wa chama hicho Rafii Kikochelo alisema amewawezeshaa
wanachama wake kuwakabidhi pikipiki na bati na kwa msaada huu
imewawezesha zaidi ya familia ya watu wanne watanufaika na mpango huu
kwa wale waliojiunga na jitihadi zaidi ya kutafuta mkopo wa zaidi ya
pikipiki 30 au 50 Kwa benki ya CRDB zinafanyika na hatua mzuri imefikia
ya kukopeshwa kwa lengo la kuwapatia wanachama wengi kuweza kupata
mkopo kwa wale wanachama hai ambao wanalipa ada ya wanachama kwa mujibu
wa katiba.
No comments:
Post a Comment