Bungeni: Serikali Kuimarisha Miundombinu Kuboresha Utalii Nchini. - LEKULE

Breaking

2 Feb 2016

Bungeni: Serikali Kuimarisha Miundombinu Kuboresha Utalii Nchini.



Serikali imejipanga kuimarisha miundombinu inayoelekea kwenye mbuga za wanyama na vituo vingine vya utalii nchini ili kuboresha utalii wa ndani na wa nje ya nchi kwa kujenga barabara ili kuwezesha watalii kufika kwa urahisi katika sehemu za vivutio vya kiutalii.

Akijibu swali la Mhe.Risala Said Kabongo Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) lililouliza serikali ina mikakati gani kuboresha miundombinu ya barabara, malazi na viwanja vya ndege katika hifadhi, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Ramo Makani amesema jitihada zimefanya na zinaendelea kufanywa ili kuboresha na kuimarisha barabara mbalimbali zinazoelekea katika hifadhi mbalimbali nchini kwa kiwango cha lami ili kuongeza wigo wa watalii kutembelea maeneo hayo kwa urahisi.

Amezitaja barabara ambazo zilizoko kwenye mpango wa kuziboreshwa ili kurahisisha watalii kuyafikia maeneo hayo kuwa ni barabara ya Sumbawanga-kasanga, barabara ya Kigoma kuelekea kusini hadi Kalya na Mwese.

“Sio tutaboresha barabara tu ila tunaviangalia pia viwanja vya ndege vinavyotumika kwa kuviimarisha na kuviboresha viwanja vya ndege vya Songwe,Kigoma na Mpanda ambavyo vitasaidia kufikika kwa urahisi maeneo ya vivutiio

“ Tunaendelea kuvutia wawekezaji binafsi kutoa huduma mbalimbali za watalii kama malazi na mpka sasa  tumetoa vibali 11 kwa wawekezaji kuwekeza katika malazi yaani Hoteli za kitalii katika Hifadhi za Ruaha,Mikumi,katavi na Mahale  na uwekezaji huo uko katika hatua za utekelezaji” Alisema Mhe. Ramo Makani.

Wizara kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na Shirika la USAID inaandaa mikakati ya kuendeleza na kuutangaza utalii kwenye maeneo mbalimbali na kuboresha miundombimu ili kuwezesha watalii kufikia vivutio kiurahisi.

No comments: