NA MWANDISHI WETU, DODOMA
BENKI ya CRDB imetoa msaada wa vifaa vya michezo kwa wabunge wa Jamhuri la Muungano wa Tanzania.
Vifaa hivyo vilikabidhiwa na Mkurugenzi wa benki ya CRDB Tawi la
Dodoma, Rehema Hamis na kupokelewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Vifaa vilivyokabidhiwa ni jezi seti mbili ikiwamo ya golikipa,
viatu, mpira, soksi na suti za michezo ambavyo vimegharimu zaidi ya Sh.
Milioni 5.
Awali Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, aliwapongeza wafadhili na
wadhamini wanaojitokeza kusaidia sekta ya michezo na kuwataka wengine
waige mfano huo, kwani hivi sasa michezo ni uchumi.
Kwa upande wake Mkurugenzi kutoka makao makuu ya CRDB
anayeshughulikia Mikakati na Ubunifu, Goodluck Nkini, alisema wameamua
kutoa vifaa hivyo kutokana na mapenzi yao kwa wananchi hususan wateja
wao, ambao wabunge ndio wawakilishi wao.
“Pia ni katika mpango wa taasisi kuunga mkono katika kazi, kwani
michezo mbali ya burudani hujenga afya, hivyo wabunge na wafanyakazi wa
CRDB wakiwa na afya njema watatekeleza vema majukumu yao,” alisema
Nkini.
Jioni ulipigwa mchezo wa kirafiki kati ya Bunge FC na CRDB kwenye Uwanja wa Jamhuri na kumalizika sare ya bao 1-1.
Walikuwa ni CRDB walioanza kuzifumania nyavu za Bunge FC dakika ya 49 mfungaji akiwa Faisal Mbuya.
Bunge FC walicharuka na kuwachukua dakika sita tu kuchomoa dakika
ya 55 kwa bao la Yusuf Gogo. Hadi mwamuzi Peter Mdachi akipuliza kipenga
kuashiria dakika 90 kumalizika, hakuna aliyeibuka mbabe.
Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Dodoma, Rehema Hamis akizungumza kabla ya kukabidhi vifaa vya michezo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia) akipokea msaada wa vifaa vya
michezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Dodoma, Rehema
Hamis kwa ajili ya timu ya soka ya Bunge. Makabidhiano hayo yalifanyika
kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma mwishoni mwa wiki. Wa pili kulia
ni Naibu Spika Dk. Tulia Akson, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa na
kushoto ni Mkurugenzi wa Mikakati na Ubunifu wa Benki ya CRDB, Goodluck
Nkini.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea viatu vya michezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Dodoma, Rehema Hamis.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia) akipokea msaada wa vifaa vya
michezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Dodoma, Rehema
Hamis kwa ajili ya timu ya soka ya Bunge. Makabidhiano hayo yalifanyika
kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma mwishoni mwa wiki. Wa pili kulia
ni Naibu Spika Dk. Tulia Akson, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa na
kushoto ni Mkurugenzi wa Mikakati na Ubunifu wa Benki ya CRDB, Goodluck
Nkini.
Waziri Mkuu akipokea mpira.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimshukuru Mkurugenzi wa Mikakati na Ubunifu wa Benki ya CRDB, Goodluck Nkini.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimshukuru Meneja wa Biashara wa Benki ya CRDB, Daniel Shemdoe.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wakurugenzi wa Benki ya CRDB pamoja na maofisa wa benki hiyo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Dodoma, Rehema Hamis.
Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Dodoma, Rehema Hamis
akimsiliza kwa makini Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa benki, hiyo, Willy
Kamwela.
Baadhi ya wachezaji wa timu ya Benki ya CRDB wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mechi yao na Wabunge.
Baadhi ya wachezaji wa Benki ya CRDB wakitoka uwanjani.
Wachezaji wa Bunge FC wakiwa katika mazoezi.
Naibu Spika Dk. Tulia Akson akikagua timu ya Benki ya CRDB.
Naibu Spika Dk. Tulia Akson akikagua timu ya Bunge.
Kikosi cha timu ya Bunge.
Kikosi cha timu ya Benki ya CRDB.
Nahodha wa timu ya Bunge, William Ngeleja (kushoto), akichuana na
mchezaji wa Benki ya CRDB, Chande Ismail katika mchezo wa kirafiki
uliofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma timu hizo zilitoka
sare ya 1-1.
Nahodha wa timu ya Bunge, William Ngeleja akimiliki mpira. Kulia ni Chande Ismail.
Mbunge wa Kilolo, Venance Mwamoto akimiliki mpira.
No comments:
Post a Comment