BAKWATA Waunga Mkono Uchaguzi wa Marudio Zanzibar - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Tuesday, 2 February 2016

BAKWATA Waunga Mkono Uchaguzi wa Marudio ZanzibarWAKATI Chama  cha wananchi CUF ambacho ni chama kikuu cha Upinzani visiwani Zanzibar kikiwa kimesusia uchaguzi wa marudio ambao unafanyika Marchi 20 ya mwaka huu,Baraza la Waislam  (BAKWATA)  limesema marudio ya  uchaguzi huo ndo njia ya kipee ya kurudisha amani visiwani humo..

Akizungumza na waandishi wa habari leo,Jijini Dar es Salaam, Sheikh Mkuu mkoani hapa,heikh alhadj Mussa Salum  amesema  Bakwata wanaunga mkono Tangazo la ZEC la kurudiwa kwa uchaguzi hu.
 
“Uchaguzi huu wa marudio  kwetu Bakwata tunaona ndio njia ya kipekee ya kukiweka kisiwa cha Zanzibar kuwa sehemu ya Amani na utulivu,natumia nafasi hii kuwaomba chama cha CUF kushiriki uchaguzi huu” Amesema Sheikh Salum.

Sheikh Salum ameongeza kwa kusema  kuwa hata kiongozi wa jumuiya ya Uamsho Visiwani Zanzibar, Sheikh Farid Hadi Ahmad amemwandikia barua na kumweleza kuwa kurudiwa kwa uchaguzi kutasaidia kurudisha Amani visiwani humo.
Katika hatua nyingine, Baraza hilo limeipongeza serikali ya awamu ya tano kwa jitihada mbalimbali inazofanya za kuimarisha nidhamu, kubana matumizi na kukuza uchumi.

"Pia tunaipongeza serikali ya awamu ya tano, inayoongozwa na Mh. John Magufuli, kutokana na hatua mbali mbali inazozichukua zenye lengo la kuimarisha nidhamu hasa kwa watumishi wa umma, hatua mabazo zimeanza kuleta tija kubwa ka taifa letu kama wote hivi leo tunavyoweza kushuhudia jinsi pato la serikali likongezeka mwezi hadi mwezi”, alisema Sheikh alhadj Mussa Salum  na kuongeza;

“Aidha tunaipongeza kwa dhamira yake ya kubana na kupunguza matumizi ya serikali, na badala yake kuelekeza fedha kwenye huduma za jamii na watanzania tumeshaanza kunufaika na huduma hizo kama vile suala la elimu bure."

 
Post a Comment