Saa chache baada ya mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi kwa mwaka 2016 kumalizika, kwa klabu ya Mtibwa Sugar ya Manungu Turiani kuibuka na ushindi wa goli 1-0 na kuweka rekodi ya kuingia fainali yake ya tano ya michuano hiyo.
Usiku wa January 10 klabu ya Dar Es Salaam Young African nayo ilishuka dimbani kucheza mchezo wa nusu fainali ya pili dhidi ya klabu ya URA ya Uganda katika dimba laAmaan, mchezo ambao ulikuwa unamtafuta bingwa mmoja kati ya timu hizo kwenda kucheza dhidi ya Mtibwa Sugar katika hatua ya fainali ya michuano hiyo.
Yanga ambayo ilikuwa inaongoza katika msimamo wa Kundi A ilianza kwa kupachika goli la uongozi dakika ya 13 kupitia kwa Amissi Tambwe ambaye aliutumia vyema mpira uliopigwa kichwa na Simon Msuva na kushindwa kutinga nyavuni, kipindi cha pili URAwaliendelea kuwa na nidhamu ya mchezo, licha ya kuwa walikuwa nyuma.
URA walifanikiwa kupata goli la kusawazisha dakika 14 kabla ya mchezo kumalizika kupitia kwa Peter, hadi dakika 90 zina malizika Yanga 1-1 URA. Katika hatua ya mikwaju ya penati Geofrey Mwashiuya na Malimi Busungu walikuwa hawana bahati, kwani walikosa penati, lakini URA mchezaji aliyekosa penati alikuwa ni Sekito Sam pekee. URAimeifuata Mtibwa Sugar fainali kwa kuibuka na ushindi wa penati 4-3.
No comments:
Post a Comment