Maamuzi mapya ya Kocha wa Taifa Stars dhidi ya Mbwana Samatta siku mbili baada ya ushindi wa tuzo (+Audio) - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Sunday, 10 January 2016

Maamuzi mapya ya Kocha wa Taifa Stars dhidi ya Mbwana Samatta siku mbili baada ya ushindi wa tuzo (+Audio)

Siku mbili baada ya mshambuliaji kimataifa wa Tanzania anayekipiga katika klabu ya TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mbwana Samatta atangazwe na shirikisho la soka barani Afrika CAF kuwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Afrikawa mwaka 2015 kwa wachezaji wanaocheza Ligi za ndani ya Afrika.
mkwasaa
Charles Boniface Mkwasa
January 10 uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Charles Boniface Mkwasa ametangaza kumteua Mbwana Samatta kuwa nahodha mpya wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars. Uamuzi huo wa Mkwasaumekuja siku mbili baada ya Samatta kutwaa tuzo. Kwa sasa Nadir Haroub atakuwa nahodha wa timu ya CHAN na John Bocco atakuwa nahodha msaidizi wa Samatta.
501184166-2
“Ni mabadiliko ya kawaida hasa baada ya Mbwana kutwaa tuzo na heshima kubwa kwa Afrika, sisi tumeona tumuongezee majukumu mengine ili aweze kutuongozea timu yetu ya taifa Taifa Stars, ameweza kuiongoza TP Mazembe kuwa Bingwa wa Afrika, hivyo tumeona tumpe fursa hii ili awaongoze wenzake katika mechi za AFCON zilizobaki” >>>Mkwasa
Unaweza msikiliza hapa Charles Mkwasa

Post a Comment