Watu wawili Wafariki Dunia na Wengine 36 Wajeruhiwa katika Ajali ya Basi la BM Morogoro. - LEKULE

Breaking

24 Jan 2016

Watu wawili Wafariki Dunia na Wengine 36 Wajeruhiwa katika Ajali ya Basi la BM Morogoro.



Watu wawili wamefariki dunia na wengine 36 kujeruhiwa, kati yao wanne vibaya baàda ya basi walilokuwa wakisafiria kutokea jijini Dar es Salaam kuelekea Morogoro, mali ya kampuni ya BM kuligonga ubavuni lori lililokuwa likija mbele yake na kuangukia kwenye bonde pembeni ya barabara na kupinduka mara nne, katika eneo la Lubungo Mikese, barabara  kuu ya Morogoro-Dar es Salaam.


Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paulo akizungumzia ajali hiyo, amesema chanzo ni mwendo kasi na imetokea majira ya saa 3:30 usiku wa kuamkia leo  ikihuhusisha basi la mwisho kutoka jijini Dar es Salaam kwenda Morogoro, mali ya kampuni ya BM, baada ya dereva wake kufika Lubungo eneo lenye kona na mteremko mkali, na akiwa mwendo kasi, kukutana mbele na lori likiwa na tela, likitokea uelekeo wa Morogoro kuelekea Dar es Salaam, likiwa linamalizia kupita lori jingine lililokuwa limeegesha barabarani baàda ya kuharibika, ambapo dereva wa basi aligonga tela la lori hilo lililokuwa kwenye mwendo na kukosa uelekeo na kupindukia bondeni na kusababisha vifo na majeruhi hao. 


No comments: