Watu 30 Wameokolewa Baada ya Kivuko cha Kilombero Kupinduka Jana Usiku.....Mtu Mmoja Hajapatikana Hadi sasa - LEKULE

Breaking

28 Jan 2016

Watu 30 Wameokolewa Baada ya Kivuko cha Kilombero Kupinduka Jana Usiku.....Mtu Mmoja Hajapatikana Hadi sasa



Watu wapatao 30 wameokolewa mpaka sasa baada ya kivuko cha mto Kilombero kushindwa kuhimili upepo mkali ulioambatana na mvua ya radi  na  kukifanya kigonge nguzo za pembeni ya mto na kukosa mwelekeo hivyo kupinduka ndani ya maji jana usiku.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya serikali iliyotolewa leo Bungeni na Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge,Kazi,Vijana ,Ajira na Walemavu) Jenista Mhagama, kivuko hicho kilikuwa  na  watu 31,magari na mizigo mbalimbali  ambapo  mpaka sasa  mtu  mmoja badohajapatikana.

Tukio la kivuko hicho cha mto Kilombero kushindwa kumudu upepo sio mara ya kwanza kujitokeza katika eneo hilo la mpakani mwa wilaya za Kilombero na Ulanga, ambapo juzi hali kama hiyo ilijitokeza.

No comments: