Mkuu wa Ujumbe wa Shirika la Fedha Duniani, IMF, Hervé Joly amesema Matarajio ya kiuchumi ya Tanzania yanatia matumaini sana, huku serikali ya awamu ya tano ikiwa imeahidi kulipa malimbikizo kwa wanaotoa huduma.
Bw.Joly amesema IMF imekamilisha tathmini ya tatu ya uchumi wa Tanzania kupitia mfumo wa PSI,ambao mapendekezo yake yanategemewa na wahisani.
Mkuu huyo wa IMF,amesema hali ya kiuchumi nchini Tanzania ni nzuri, na uchumi ukiwa umekuwa kwa asilimia 7 mwaka 2015 na ongezekeo la bei za bidhaa likiwa ni asilimia 5.6 tu.
Licha ya hayo, amesema IMF imekuwa na wasiwasi kuhusu bajeti ya serikali lakini amesema harakati zilizochukuliwa na serikali mpya zimetia matumaini.
Amesema matarajio ya ukuaji wa uchumi ni mazuri kwa mwaka 2016,huku IMF ikipendekeza kuendelea kuleta mabadiliko katika matumizi ya serikali na hasa kupunguza madeni ya TANESCO.
No comments:
Post a Comment