UMAARUFU wa Sheikh Chief Msopa - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Wednesday, 13 January 2016

UMAARUFU wa Sheikh Chief MsopaUMAARUFU wa Sheikh Chief Msopa maarufu kwa jina la Sharif Majini kwa sasa unazidi kushika kasi nchini Tanzania na nchi za Afrika Mashariki kwa ujumla. Sharif Majini ameamua kutumia Kituo cha Dua kilichopo Mabibo Mwisho Dar es Salaam, kwa ajili ya kufanya dua na maombi kwa kusaidia wenye shida mbalimbali.

Kwa sehemu kubwa dua na maombi yake yamekuwa msaada mkubwa kwa wenye matatizo mbalimbali. Dua hizo kwa sehemu kubwa zinasaidia kwa wenye matatizo mbalimbali ya kiafya. Hivyo, wengi wanaofika kwenye kituo hicho ni kwa ajili ya kutatua shida hizo. Sharif Majini anatumia dua kwa ajili ya kusaidia wale ambao wana matatizo ya kupooza viungo vyote muhimu na kuwa na maumivu kama kuumwa kichwa.Pia kwa kutumia dua zake na maombi kwa ajili ya kusaidia wenye tatizo la mimba kuharibika mara kwa mara. Waliokosa kasi na wanaoandamwa na mikosi kwenye maeneo wanayoishi na wale wenye tatizo la kupata hedhi muda mrefu.

Pamoja na hayo Sharif Majini kwa kutambua kuwa kuna umuhimu wa dua na maombi yake kusaidia watu wengi ameamua kuifanya siku ya Jumapili kuwa siku ya kufanya dua na maombi maalumu kwa wale ambao wanakosa nafasi ya kwenda kutokana na majukumu mengine yakiwamo ya ujenzi wa taifa.Hivyo, Sharif Majini kwa sehemu kubwa kupitia dua zake amefanikiwa kusaidia wananchi wengi hasa wa Dar es Salaam na mikoani ambao wamekuwa wakisumbuliwa na maradhi. Mbali ya wale wanaofika kwenye vituo hivyo, Sharif Majini amekuwa akitumia karama hiyo aliyopewa na Mungu kuitumia kwa ajili ya kuliombea Taifa lake liendelee kuwa na amani na utulivu ili maisha ya ujenzi wa nchi yaendelee.

Mbali ya kufanya maombi kwa viongozi wa ngazi mbalimbali kwa kutenga siku maalumu kwa ajili ya kuwaombea kwa Mungu, pia Sharif Majini amekuwa akifanya dua na maombi kwa ajili ya viongozi wa nchi nyingine nyingi za Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla na hiyo inatokana na mialiko ambayo amekuwa akiipata. Siku za karibuni licha ya kufanya mambo kwa ajili ya wananchi wanaofika kwa wingi kwenye kituo kipya cha dua, aliamua kutumia uwezo wake ambao amejaliwa na Mungu kufanya dua maalumu ya kumuombea Rais, Dk. John Magufuli. Dua hiyo kwa sehemu kubwa ililenga kumuomba Mungu ampe nguvu na afya njema Rais ili kutimiza majukumu yake. Pia kumuomba Mungu kumuepusha na mabaya hasa kipindi hicho ambacho ameamua kupambana na ufisadi na kutumbua majipu.

Siku za karibuni Jambo Leo liliamua kufanya naye mahojiano Sharif Majini baada ya kupata taarifa za dua na maombi anayofanya kuonekana kusaidia wakazi wengi wa Dar es Salaam ambao kwa sehemu kubwa wanakwenda kwa ajili ya kuondolewa majini na matatizo mengine ya maradhi. Hadi sasa zaidi ya nchi 40 za Afrika amekwenda kufanya maombi kutokana na mialiko ya wananchi wa dini zote na viongozi kadhaa. Kote ambako amekwenda amekuwa na mafanikio makubwa.

Wanaopata dua na maombi yake wanafanikiwa. Hili ni jambo ambalo limemfanya Sharif Majini kuamua kutumia nafasi hiyo kuendelea kutoa dua na maombi kwa kadri anavyoweza kulingana na uwezo ambao Mungu amempa. Akizungumza kwa kujiamini akiwa kwenye Kituo chake cha maombi Mabibo Dar es Salaam , Sharif Majini anaanza kwa kueleza kuwa anamshukuru Mungu kwa kumpa uwezo wa kufanya dua na maombi ambayo yanakuwa msaada kwa wenye shida.

Hivyo, jukumu lake kubwa ni kutumia kituo chake cha dua na maombi kusaidia wenye shida hiyo na kueleza kwa Dar es Salaam uchunguzi wake umebaini nusu ya wakazi wanakabiliwa na maradhi yanayosababishwa na majini lakini wasiwe na hofu maana kazi ya kuyatoa anaiweza kutokana na kipaji cha dua alicho nacho.

"Kwanza naomba ifahamike kuwa kituo chetu ni kwa ajili ya maombi na dua na hivyo hatutoi tiba maana hiyo si kazi yetu. Hivyo, kwa wale ambao wanakuja kwetu ninachokifanya ni kumuomba Mungu kupitia dua na wamekuwa wakipata wakipona maradhi na kwa wale wenye majini na mapepo nao wamekuwa wakibaki salama,"anasema Sharif Majini.

Sharif Majini anasema tangu kuanza kutoa dua na maombi alichobaini ni kwamba kuna wananchi wengi wanakabiliwa na maradhi ambayo kimsingi ni majini na mapepo ambayo yapo kwenye miili yao. Anasisitiza kuwa katika kutoa majini, Sharif Majini anatumia dua na mambo maalumu na kabla ya hapo anatoa supu maalumu ya ajabu ya kutoa siniri mwilini. Akifafanua zaidi kuhusu huduma anayotoa, Sharif Majini anaeleza wazi anajisikia faraja pale anapoona wanaofika kwenye kituo hicho wakiwa na matatizo makubwa lakini baada ya dua na maombi wanaondoka wakiwa na matumaini mapya.

Hivyo, anasema kuanzia hapo, dua zake zikaanza kupata umaarufu mkubwa kwenye nchi hiyo na kusababisha kueneoe kwenye nchi nyingine mbalimbali barani Afrika na Asia."Huwa nafarijika baada ya kufanya maombi kwa wenye maradhi mwilini na kisha wakapata nafuu. Natambua nimekuwa nikiponya wengi kwa kutumia dua. Hili ni jambo la kumshukuru Mungu kwani natoa huduma kwa jamii kwa kutumia njia hii ya kutatua shida za walio wengi,"anasisitiza.

Alipoulizwa ni lini alianza kujihusisha na utoaji maombi na dua, Sharif Majini anasema kwa muda mrefu amekuwa akifanya dua kwa ajili ya wenye shida na alianza kupata umaarufu baada ya kumfanyia dua aliyekuwa Rais wa Zambia Fredrick Chiluba ambaye kwa sasa ni marehemu. Hiyo ilikuwa ni mwaka 1999. Anasema alikwenda kwenye nchi hiyo baada ya mualiko maalumu wa rafiki yake Yusuph Chifili aliyekuwa mwanasiasa mwandamizi kwenye nchi hiyo na hivyo baada ya kuona dua zake zinasaidia wananchi wengi a nchi hiyo ndipo Chiluba aliapoamua kumualika Ikulu kwa ajili ya maombi.Sharif Majini anasema tangu kipindi hicho pamoja na kutoa huduma nyingine kwenye jamii, bado muda wake mwingi unatumika kwa ajili ya kufanya dua na maombi kwa wenye shida mbalimbali.

Sharif Majini anasema kwa kutambua umuhimu wa kuwa na afya njema na watu kuwa na utulivu wa akili na mwili, ndiyo maana akaamua kuweka siku maalumu kwa ajili ya dua ambayo ni Jumapili ili siku nyingine zitumike kwa watu kufanya kazi huku wale wenye muda wakipatiwa dua wakati wowote. Hivyo, uamuzi wake wa kuwa na kituo cha dua Dar es Salaam umerahisisha kwa wenye kumhitaji kumuona kuwa na urahisi tofauti na ilivyokuwa awali ambapo alitoa dua kutokana na maombi maalumu.

 Anasema tangu akiwa mdogo amekuwa akijihusisha na mambo ya dini, na hiyo imemwezesha kuwa na karama ya hali ya juu ya kusaidia kusoma dua na kusaidia wenye maradhi mwilini.Anatumia nafasi hiyo kusisitiza kuwa yeye amekuwa akifanya dua na si uganga maana kuna tofauti kubwa kati ya mwenye kufanya dua na mwenye kufanya uganga. Kwa kutumia dua zake amekuwa akisaidia watu wa rika tofauti na wenye vipato tofauti.

 Uchunguzi wake umebaini asilimia 85 ya wanaopata maombi yake wanapona maradhi yanayowasumbua. Anatumia nafasi hiyo kusisitiza pamoja na kutumia muda wake kwa ajili ya kuwafanyia dua wenye dhida, bado anaona umuhimu kwa Watanzania kuendelea kutunza amani ya nchi na kutumia utulivu uliopo kwa ajili ya kushiriki kwenye uchumi wa nchi yetu. 
Post a Comment