TAARIFA KWA UMMA
Taarifa hizo siyo sahihi na wananchi wanatakiwa kupuuza upotoshaji huo wenye sura ya utapeli unaofanywa na kikundi kidogo cha watu. Aidha, yeyote anayedai kupewa fedha ili aweze kumuingiza kijana katika Jeshi la Kujenga Taifa aripotiwe mara moja Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa.
Katika hili unahitajika ushirikiano wa karibu sana ili kuweza kudhibiti udanganyifu na utapeli unaofanywa na watu wachache wanaojifanya wana uwezo wa kuwaingiza vijana JKT, na kudai watumiwe fedha kupitia mitandao ya simu za mikononi kama vile Tigo Pesa, M- Pesa, Airtel Money.
JKT linasisitiza kuwa, muda wa kuanza mchakato wa kuchukua vijana wa kujiunga na mafunzo ya JKT kwa kujitolea utakapowadia, wananchi watatangaziwa rasmi kupitia Mamlaka za Serikali zinazohusika pamoja na vyombo vya habari hapa nchini. Aidha inazidi kukumbushwa kuwa nafasi za vijana kujiunga na mafunzo ya JKT kwa kujitolea hazipatikani kwa kununuliwa.
IMETOLEWA NA
KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO,
MAKAO MAKUU YA JESHI LA KUJENGA TAIFA,
LEO TAREHE 08 JANUARI 2016
kwa maelezo na uhakika zaidi tembelea hapa
http://www.jkt.go.tz/component/k2/item/587-taarifa-kwa-umma.html
No comments:
Post a Comment