SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LASHINDA TUZO YA HESHIMA KATIKA UVUMBUZI - LEKULE

Breaking

19 Jan 2016

SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LASHINDA TUZO YA HESHIMA KATIKA UVUMBUZI

ETIHAD imetunukiwa tuzo ya kifahari ya “Uvumbuzi katika Usafiri” katika hafla iliyoandaliwa na jarida la Travel Weekly ya kuwatunza wadau wa sekta ya usafiri dunia nzima huko Uingereza maarufu kama “Globe Travel Awards”. Hafla hiyo ilifanyika katikati ya wiki kwenye hoteli maarufu ya Grosvenor House, iliyopo Jijini London.

Kwa kawaida tuzo hii hupewa kampuni ambayo imevumbua bidhaa au huduma yenye kuleta wimbi la mabadiliko na maendeleo katika soko. Shirika la Etihad waliibuka washindi baada ya jopo la wataalamu kuamua kwamba Shirika linastahili tuzo hii kutokana na huduma yake ya “Makazi”- ambayo ni huduma binafsi ya kipekee duniani yenye kutoa vyumba vitatu kwenye ndege ya Etihad. Huduma hii, iliyoleta mapinduzi katika sekta ya usafiri wa anga,ni matokeo ya programu ya utafiti na maendeleo iliyoendeshwa kwa miaka saba na kusimamiwa na timu nzima ya ubunifu kutoka kituo cha Uvumbuzi, Jijini Abu Dhabi.
“Makazi” yanayopatikana kwenye ndege za Etihad aina ya Airbus A380 yana ukubwa wa mita za mraba 11 na ndani yake kuna sebule, bafu la pembeni, chumba kikubwa cha kulala na mhudumu mmoja kwa kila chumba.
Shane O’Hare, Makamu Rais wa Masoko wa Shirika la ndege la Etihad alisema: “Tunafurahishwa na uamuzi wa jopo la wataalamu wa tuzo za Globe Travel, ambao ndio walipiga kura ‘Makazi’ kuwa huduma bora iliyovumbuliwa katika sekta yetu. Vyumba hivi vimebadili mitazamo ya wengi, vikiwapa fursa watu wa kawaida kufurahia huduma zinazopatikana mara nyingi katika ndege binafsi tu.”
“Etihad inathamini ushirikiano kati yake na soko la Uingereza, uhusiano ulioanza tulipozindua safari zetu kuelekea na kutoka uwanja wa ndege wa Heathrow uliopo jijini London mnamo mwaka 2004. Tumeinua hadhi ya usafiri ikiwa ni pamoja na kuzipa ndege zetu muonekano halisia wa makazi ya kuishi na kuwapa wasafiri viwango vya hali ya juu vya faragha na utulivu”.
Huduma ya ‘Makazi’ inapatikana ndani ya ndege aina ya A380 zinazofanya safari zake kati ya Abu Dhabi na London, New York pamoja na Sydney. SHirika la Etihad linatazamia kuzindua huduma hii katika ndege ziendazo Mumbai na Melbourne mwaka huu.
Etihad ina timu maalumu ambayo kazi yake pekee ni kuhakikisha wanaochagua kusafiri na ndege zao wanaweza kufuruahia vyumba ya ‘Makazi’ wapendavyo. Timu hii pia ipo karibu na watoa huduma maalum waliopo kwenye vyumba hivi. Wateja wanapewa fursa ya kufurahia huduma mbalimbali wakiwa wanasafiri na ndege hii ya Etihad zikiwemo; kuweka oda ya mahala pa kula, burudani ndani ya ndege, matukio maalum kama sherehe za kuzaliwa, maelezo kuhusu waendako na kadhalika. Watuapo, timu hiyo maalum (VIP) huwasaidia wageni katika kufanya taratibu za kuwasili na usalama.

Ndege za Etihad zinafanya safari zake kwenda Uingereza kutwa mara sita, pamoja na kutoa huduma za safari za moja kwa moja kati ya uwanja wa ndege wa Heathrow uliopo jijini London na kuelekea Machester na Ediburgh, zilizoanzishwa Juni 8 mwaka jana. Uwanja wa ndege wa Heathrow ulipewa nafasi kuwa kiwanja cha kwanza ndege aina ya Airbus A380 za Etihad kutua kwa mara ya kwanza, na hivyo huduma hiyo ilianza mwishoni mwa mwaka 2014.

No comments: