Serikali yasitisha ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo, yajielekeza kuziimarisha Bandari za Dar na Mtwara - LEKULE

Breaking

8 Jan 2016

Serikali yasitisha ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo, yajielekeza kuziimarisha Bandari za Dar na Mtwara

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema ujenzi wa bandari ya Bagamoyo utasubiri hadi kukamilika kwa uongezaji wa kina cha maji katika Bandari ya Dar es Salaam na uboreshaji wa Bandari ya Mtwara.
Profesa Mbarawa alisema mbali ya kuongeza kina katika bandari ya Dar es Salaam, pia kipaumbele kikuu ni kujenga gati namba 13 na 14 zinazopigiwa kelele.
Akizungumza jana katika ofisi za Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa), Profesa Mbarawa alisema mkakati wa Serikali kwa sasa ni kuhakikisha Bandari ya Dar es Salaam, gati namba moja hadi namba saba zinaongezwa kina cha maji ili kuongeza ufanisi.
Alisema lengo la ziara yake katika ofisi hizo ni kujifunza na kuzungumza na wafanyakazi huku akisisitiza uwajibikaji.
Akielezea kuhusu kukwama kwa kivuko cha Mv Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mhandisi Joseph Nyamhanga alisema ni miundombinu ya kukiendesha ikiwamo vituo kwa ajili ya kupandisha na kushusha abiria.

Alisema tayari fedha zimepatikana na wanaanza ujenzi wa kituo cha kwanza eneo la Jangwani Beach na baadaye Ununio.

No comments: