Serikali
kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu maafa imeanza mkakati wa
menejimenti ya maafa ya ukame kwa kuwawezesha wananchi wanao kabiliwa
na njaa kuweza kukabili maafa hayo kwa kuwagawia wananchi hao mbegu bure
za mazao yanayohimili ukame katika halmashauri husika.
Kufuatia
hali ya ukame ambao umezikumba baadhi ya halimashauri hapa nchini
katika msimu wa 2014/2015, baadhi ya halmashauri hizo zilipata upungufu
wa chakula hali iliyopelekea halmashauri hizo kuomba chakula cha msaada
Ofisi ya Waziri Mkuu Idara ya Uratibu maafa.
Akiongea
wakati wa ziara ya kukagua hali ya upungufu wa chakula katika kata ya
Malengamakali, wilayani Iringa Tarehe 11 Januari, 2016, Mkurugenzi wa
Idara ya uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Jenerali Mbazi
Msuya amebainisha kuwa mkakati uliopo ni kuwahamasisha wananchi walime
mazao yanayohimili ukame.
“Nashauri
watendaji wakuu wa Halmashauri na mikoa kupitia kamati za maafa
waorodheshe wananchi wote wanaohitaji mbegu hizo na kuwasilisha katika
Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu maafa na Ofisi yangu itatuma
fedha za kununua mbegu hizo ili zigawiwe bure kwa wananchi wengine wenye
upungufu wa chakula, tunahitaji wananchi wote wawe na uhakika wa
chakula .” amesema Brig. Jen. Msuya.
Awali
akiongea katika ziara hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Halmashauri ya Iringa,
Richard Kasesela, alibainisha kuwa katika kukabiliana na upungufu wa
hali ya chakula halmashauri hiyo imefanya uhamasishaji wa kilimo cha zao
la Mtama amabalo ni zao linalovumilia ukame na mazao mengine
yanayokomaa kwa muda mfupi kama vile viazi vitamu.
“Uhamasishaji
umefanyika katika Tarafa za Isimani, Idodi, Pawaga na Kalenga (mfyome),
tumeanzisha na sheria ndogo ya kilimo ambayo inaitaka kila kaya kulima
mtama ekari mbili katika kata hizi na atakayekiuka sheria hii adhabu
yake ni kulipa kiasi cha fedha shilingi 50,000/=” alisisitiza Kasesela.
Katika
kukabiliana na upungufu wa chakula Halmashauri ya Iringa iliomba
chakula cha msaada kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu Maafa,
ikiwa hadi kufikia Disemba 2015, tayari tani 4, 546 zilikuwa zimeletwa
wiliyani humo ambazo zimesambazwa katika Kata 11, vijiji 42 katika
maeneo yenye upungufu wa chakula.
No comments:
Post a Comment