Ostaz Juma: Najivunia Miaka 10 Ya Ndoa Yangu! - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Sunday, 10 January 2016

Ostaz Juma: Najivunia Miaka 10 Ya Ndoa Yangu!OSTAZ JUMA (1)Mdau wa muziki nchini, Ostaz Juma Namusoma (kulia) akipozi na mkewe Mariam David  na mtoto wao Hayyan Juma ‘Boy’.OSTAZ JUMA (2)…Akiwa na familia yake.OSTAZ JUMA (3)…Akiwa na mkewe.OSTAZ JUMA (4) …Wakipata chakula.OSTAZ JUMA (5)…Wakiwa kwenye mtoko.

MDAU wa muziki nchini, Ostaz Juma Namusoma, ameibuka na kufunguka ya moyoni kuhusu maisha yake ya ndoa, wakati akiingia mwaka mpya 2016.

Ostaz, ambaye ni baba wa mtoto mmoja wa kiume, Hayyan Juma ‘Boy’ aliyezaa na mkewe Mariam David ‘ a.k.a Mama Boy, amesema kuwa wakati akisherehekea kumalizika na kuanza kwa mwaka mwingine wa 2016, anajivunia ndoa  yake kufikisha miaka kumi sasa.

“Ni jambo la kujivunia kufikisha takriban miaka kumi ya ndoa sasa, tena ndoa yenye amani na utulivu. Mimi na mke wangu, tumepitia matatizo na majaribu mengi, ambayo tunamshukuru Mwenyezi Mungu tumeyavuka na tunapendana sana,” alisema Ostaz wakati akiongea na Global Publishers iliyokutana naye Ramada Hotel, Mbezi Beach jijini Dar  hivi karibuni.

Akitoa salamu zake za mwaka mpya kwa wadau, ametoa wito wa kufanya kazi kwa bidii na kuachana na majungu, hasa ikizingatia kuwa tumepata kiongozi wa nchi  mchapakazi.

“Natoa wito kwa vijana wenzangu kuwa tuchape kazi tuache majungu, tumepata kiongozi mzuri (Rais Dk. Magufuli) ambaye atatusaidia vijana kutuletea maendeleo ya haraka,” alisema Ostaz.

Ostaz ni miongoni mwa wadau wa muziki nchini Tanzania ambaye husaidia kuendeleza wasanii wa muziki chini ya lebo yake ya Mtanashati Entertainment, ambapo wasanii kama PNC, Kitale na Dogo Janja wamepitia kwenye lebo hiyo.
Post a Comment