Hatimaye Wizkid kufunga ndoa! - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Sunday, 10 January 2016

Hatimaye Wizkid kufunga ndoa!Wizkid-22-600x597
Staa wa muziki kutoka Nigeria, Wizkid.

KWA mara ya kwanza staa wa muziki kutoka Nigeria, Wizkid amefunguka kuwa yupo mbioni kufunga ndoa na mchumba wake wa siku nyingi, Tania Omotayo.

Wizkid mwenye mtoto mmoja aitwaye Boluwatife amekuwa na uhusiano na Tania kwa muda mrefu na uhusiano wao umekuwa wa kuachana na kurudiana lakini amesema hilo halimpi shida kwani Tania yupo moyoni mwake na itaendelea kuwa hivyo.

Tania-and-wizkid

Alisema kuwa hajali maneno yasemwayo kwa baadhi ya wati, mara zote atabakia kuwa na Tania moyoni mwake na ataendelea kufanya kila liwezekanalo kumpa mapenzi matamtamu na wasubiri ndoa hivi karibuni. “T (Tania) ni wa moja kwa moja kwangu.”

Kila la heri, Wizkid katika ndoa yako na Tania.
Post a Comment