MUSWADA
wa Sheria ya Habari ambao uliwahi kupelekwa bungeni kisha kuondolewa
kimya kimya, sasa unatarajiwa kurejeshwa tena bungeni mwezi huu.
Uwezekano
wa kurejeshwa tena bungeni kwa muswada huo, kunatokana na kuundwa kwa
kamati ya wanahabari sita, itakayoshirikiana na Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (pichani) kupitia muswada huo
kabla ya haujawasilishwa bungeni baadaye mwezi huu.
Akizungumza
Dar es Salaam jana na wahariri wa habari wa vyombo mbalimbali vya
habari nchini, Nnauye alisema serikali inathamini mchango mkubwa wa
vyombo vya habari na watendaji wake, na kwamba itashirikiana nao
kuhakikisha sheria bora ya habari inapatikana.
Kamati
hiyo imeundwa baada ya mapendekezo ya Waziri Nnauye ambaye alitaka
kamati hiyo iundwe na ikutane naye Januari 13 mwaka huu, kwa ajili ya
kuanza kupitia muswada huo wa sheria ya habari.
Wanaounda
kamati hiyo ni Naibu Mhariri Mtendaji wa kampuni ya TSN, Tuma Abdallah,
Mhariri Mkuu wa gazeti la Nipashe, Jesse Kwayu na Mhariri Mtendaji wa
gazeti la Jamhuri, Deodatus Balile.
Wengine
ni Mhariri wa Upendo Media, Mengda Johanes, Prudence Constantine wa
Shirika la Taifa la Utangazaji(TBC1) na Joyce Shebe wa Clouds Media.
Awali,
akizungumza na wahariri hao, Nnauye alisema vyombo vya habari nchini
vina mchango mkubwa katika taifa na vinapaswa kuwa na sheria
inayowasimamia, ili kuhakikisha uhuru wa habari unakuwepo na pia kuwa
kuwa na mipaka yake.
Nape
aliongeza kuwa yeye ni muumini mzuri wa uhuru wa habari nchini, hivyo
atahakikisha anatekeleza wajibu wake kwa kuharakisha mchakato wa muswada
wa sheria hiyo, kwa kuhusisha wadau watoe mapendekezo kabla ya
kuupeleka bungeni.
Alisema
nia ya serikali kutunga sheria hiyo ni nzuri kwa kuwa inaweka utaratibu
wa kurahisisha utekelezaji wa majukumu ya vyombo vya habari ili kuwa na
mazingira mazuri na yenye tija.
Akizungumzia
masuala ya vitambulisho vya waandishi (press card), Nnauye alitoa wiki
moja kwa Idara ya Habari (Maelezo) kuangalia kanuni na utaratibu mzuri
wa jambo hilo na kutoa mwongozo utakaotumika kwa ajili ya utoaji
vitambulisho hivyo na kwa muda gani.
“Nawapa
siku saba Maelezo, mkakae, muangalie kanuni na taratibu zikoje, ili
mniletee ripoti juu ya jambo hili,” alisema Waziri Nnauye.
Kuhusu Muswada wenyewe
Katika Bunge la Juni mwaka jana, serikali iliuondoa Muswada wa Sheria ya Haki ya Upatikanaji Habari wa mwaka 2015, uliokuwa usomwe kwa mara ya pili.
Katika Bunge la Juni mwaka jana, serikali iliuondoa Muswada wa Sheria ya Haki ya Upatikanaji Habari wa mwaka 2015, uliokuwa usomwe kwa mara ya pili.
Ilieleza kuwa muswada huo utasubiri bunge jipya litakapokaa, baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka 2015.
Akitoa
taarifa ya kuondolewa kwa muswada huo bungeni mbele ya Naibu Spika, Job
Ndugai (wakati huo), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu), kwa
wakati huo, Profesa Mark Mwandosya alisema, “Uamuzi wa kuuondoa
umeafikiwa na Serikali baada ya Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Huduma za
Jamii kuishauri hivyo.”
Mwandosya
alisema sheria hiyo ya upatikanaji habari ilichapishwa Februari 20
mwaka 2015 na kusomwa bungeni kwa mara ya kwanza Machi 12 hadi Aprili
mosi mwaka huo.
Alisema muswada huo si wa dharura, kwa kuwa umepitia hatua mbalimbali, ikiwemo kujadiliwa na kamati hiyo Juni 22.
No comments:
Post a Comment