Mbunge wa
Kinondoni, Maulid Mtulya akipata maelezo kutoka kwa wakili
anayesimamia kesi ya Msingi kwa wakazi wa Mabondeni kupinga kubomolewa
nyumba zao, muda mfupi baada ya Jaji wa Mahakama Kuu ya Ardhi kutoa
hukumu ya maombi ya waombaji hao ambapo Jaji huyo ametoa kwa siku 60,
nyumba hizo zisibomolewe na baada ya hapo mambo mengine ya kisheria
yanaweza kufuata zaidi ikiweo kukata rufaa kwa pande zote mbili ikiwemo
Serikali na walalamikaji hao. (Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog)
Mbunge wa
Jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulya (CUF) akitoka katika Mahakama kuu ya
Ardhi, baada ya kutolewa kwa hukumu juu ya kesi yao ya msingi ya kupinga
kubomolewa nyumba za wananchi wa mabondeni ambapo Jaji wa Mahakama hiyo
ametoa maamuzi ya siku 60 pekee kudumu kwa kusimamisha zoezi la
ubomoaji na baada ya hapo maamuzi mengine yafuate.
Mbunge wa
jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulya akitoa ufafanuzi kwa wanahabari na
wananchi wa mabondeni waliofurika kusikiliza kesi yao hiyo mapema leo.
Wananchi hao wakimsikiliza mbunge wao huyo akitoa ufafanuzi wa kile kilichoamuliwa dhidi ya Mahakama kuu ya Ardhi.
Hata
hivyo, Upande wa Mawakili wanaotetea kesi dhidi ya wananchi wa mabondeni
wamebainisha kuwa, katika kuhakikisha haki inatendeka, kwa sasa
wanapitia vifungu vya kisheria zaidi ilikuona wanachukua hatua gani
katika kuhakikisha wanawapatia haki wananchi hao.
Kwa
upande wake, Mbunge huyo ambaye aliweza kufika leo kwa dharura akitokea
Bungeni mjini Dodoma, alifika Mahakamani hapo majira ya mchana wa saa
huku kesi hiyo ikianza saa 10 kaso robo na kudumu kwa saa moja na na
robo, na kuamua Jaji Kente wa mahakama hiyo kutoa hukumu hiyo ambapo pia
amezitaka pande zote kuwa zinazo haki ya kukata rufaa zaidi pindi
watakapoona hawajatendewa haki.
No comments:
Post a Comment