KILELE CHA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 52 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR. - LEKULE

Breaking

12 Jan 2016

KILELE CHA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 52 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR.


 Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akisalimiana naRais Mstaafu wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo katika killele cha sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kutimia miaka 52,zilizofanyika katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja,ambapo mgeni rasmi  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
 Pichani kutoka kushoto Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi,Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein,Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange wakiwa katika kilele cha Sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kutimia miaka 52 katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja zilizofanyika leo
 Baadhi ya Wananchi na Maafisa mbali mbali wa Serikali wakiwa katika sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kutimia miaka 52,zilizofanyika leo katika Uwanja wa Amaani Studium Mjini Unguja
  Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa akisalimiana na Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu wakati alipowasili katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja katika Kilele cha sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kutimia miaka 52,ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange katika kilele cha Sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kutimia miaka 52 katika Uwanja wa Amaan Studium zilizofanyika leo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akisalimiana na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein katika kilele cha Sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kutimia miaka 52 katika Uwanja wa Amaan Studium zilizofanyika leo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia mkono wananchi walioshiriki katika kilele cha Sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kutimia miaka 52 katika Uwanja wa Amaan Studium leo akiwa katika gari maalum
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiteremka katika gari maalum alilopanda wakati akiwasalimia wananchi katika kilele cha Sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kutimia miaka 52 katika Uwanja wa Amaan Studium leo.
[Picha na Ikulu.]

No comments: