Kikao
cha kwanza cha Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar chakutana
chini ya mwenyekiti wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif
Ali Iddi ofisini kwa Vuga Mjini Zanzibar.
Balozi
Seif akikiongoza Kikao cha Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar
akisaidiwa na Makamu Mwenyekiti wake kulia, Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Moh’d Aboud Moh’d.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar Nd. Ali Juma
Hamad aliyesimama akitoa Muhtasari wa Sheria ya Kamisheni hiyo kwenye
Kikao cha kwanza Wajumbe wa Kamaisheni hiyo.
Mkurugenzi
wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Kanda ya Zanzibar Nd. Moh’d Khamis
Ngwali akitoa ufafanuzi wa muelekeo wa mvuza zinazonyesha za mwezi
januari na febuari 2016 kwenye kikao cha kwanza cha Kamisheni ya
Kukabiliana na Maafa Zanzibar.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Kikao
cha kwanza cha Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar kimeanza rasmi
ambapo Wajumbe wa Kamisheni hiyo wamekutana chini ya Mwenyekiti wake
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Kufutwa
kwa Sheria nambari 2 ya mwaka 2003 na kuanzishwa kwa sheria nambari 1
ya mwaka 2015 ya kukabiliana na maafa Zanzibar ndio iliyotoa mamlaka kwa
kamisheni hiyo kutekela majukumu yake hapa Nchini.
Akiwasilisha
Muhtasari wa sheria ya kukabiliana na maafa Zanzibar kwenye Kikao
hicho, Mkurugenzi Mtendaji wa Kamisheni ya kukabiliana na Maafa
Zanzibar Nd. Ali Juma Hamad alisema mabadiliko ya sheria hiyo yamekuja
kutokana na mapunugu kadhaa yaliyokuwa yakikwamisha utekelezaji wa
shughuli za kujikinga na kukabiliana na maafa hapa Zanzibar.
Nd.
Juma alisema kukosekana kwa muundo wa usimamizi, mfumo madhubuti wa
utoaji wa Taarifa, ushiriki wa sekta binafsi pamoja na mbinu za
kujiandaa, kujikinga na kurejesha hali ya kawaida baada ya maafa ni
baadhi ya masuala yaliyokuwa yakileta usumbufu katika kipindi
kilichopita nyuma.
Akitoa
ufafanuzi wa Taarifa ya muelekeo wa Mvua mkubwa kwa mwezi wa Januari na
Febuari mwaka 2016 Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania
Kanda ya Zanzibar Nd. Moh’d Khamis Ngwali alisema changamoto za mvua
zinazonyesha ni kiashirio kinachoweza kusababisha Mvua za Alninyo.
Nd.
Ngwali alisema kwa mujibu wa miongo ya mvua miezi ya Januari na Febuari
ni misimu ya vimbunga ambavyo vinaweza kuleta athari wakati wowote na
mamlaka hulazimika kutoa tahadhari pale mvua inapoendelea kunyesha
wakati ikipindukia zaidi ya milimita arubaini.
Naye
Waziri wa Fedha Zanzibar Mh. Omar Yussuf Mzee alisema Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar tayari imeshaandaa mfuko maalum wa Miundo mbinu
{ Infrustructure Fund } ambao huchangiwa na Kila Mgeni anayeingia
Nchini kwa Dola Moja ya Kimarekani.
Mh.
Omar alisema matarajio ya makusanyo ya mkufo huo imekadiriwa kufikia
shilingi Bilioni 25 ambapo asilimia 25% ya makusanyo hayo yamelengwa kwa
Mifuko saba iliyosajiliwa akatolea mfano kama ile ya Maafa pamoja na
ukimwi.
Wakichangia
katika Mkutano huo baadhi ya wajumbe wa Kikao walisema bado ipo haja
ya kuandaliwa njia mbadala kwa watu wanaoishi katika maeneo hatarishi
itakayokuwa ya kudumu katika kudhibiti maafa wakati yanapotokea.
Kuhusu
Kikosi cha Zima moto na Uokozi Zanzibar Wajumbe hao waliiomba
Serikali Kuu kwa kushirikiana na Taasisi za Kitaifa na Kimataifa
kukijengea uwezo zaidi wa Vifaa Kikosi hicho ili kiwe na uwezo wa
kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa zaidi.
Akitoa
nasaha zake Mwenyekiti wa Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar
ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
alisema Umoja wa Mataifa tayari umeshatoa onyo la kuziasa Nchi wanachama
kuwa tayari kukabiliana na mabadiliko ya tabia Nchi wakati wowote
yanapotokea.
Kikao
hicho cha kwanza cha Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar
kilijumuisha wajumbe mbali mbali wakiwemo Mawaziri, wakuu wa Mikoa na
Vikosi vya ulinzi pamoja na watendaji wa taasisi zinazohusiana na maafa
hapa Nchini.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
21/1/2016.
No comments:
Post a Comment