KATIBU MKUU, NAIBU KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI YA NCHI WAFANYA ZIARA JESHI LA MAGEREZA, WALIPONGEZA KWA UTENDAJI MZURI WA KAZI - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Thursday, 21 January 2016

KATIBU MKUU, NAIBU KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI YA NCHI WAFANYA ZIARA JESHI LA MAGEREZA, WALIPONGEZA KWA UTENDAJI MZURI WA KAZI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kushoto) akimsalimia Mkuu wa Jeshi la Magereza, Kamishna Jenerali (CGP), John Minja wakati alipokuwa anawasili ofisi ya Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya ziara ya kikazi. Katibu Mkuu Rwegasira alilipongeza jeshi hilo kwa utendaji wa kazi mzuri licha ya kuwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali. Kulia ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi hilo, Gaston Sanga, na anayefuata ni Kamishna wa Sheria na Utawala wa Jeshi hilo, Dk Juma Malewa.
Mkuu wa Jeshi la Magereza, Kamishna Jenerali (CGP), John Minja akitoa taarifa ya utendaji wa Jeshi lake kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati meza kuu) wakati Katibu Mkuu huyo alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu Rwegasira alilipongeza jeshi hilo kwa utendaji wa kazi mzuri licha ya kuwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali. Kushoto meza kuu ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati) akizungumza na Makamanda wa Jeshi la Magereza wakiongozwa na Kamishna Jenerali, John Minja (kushoto meza kuu) wakati Katibu Mkuu na Naibu wake walipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake, Meja Jenerali Rwegasira alilipongeza jeshi hilo kwa utendaji wa kazi mzuri licha ya kuwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kulia) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza mazungumzo na Makamanda wa Jeshi la Magereza wakiongozwa na Kamishna Jenerali, John Minja (wapili kulia) wakati Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu huyo walipofanya ziara ya kikazi ofisi za Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake, Balozi Simba alilitaka jeshi hilo wawatumie wafungwa wenye makosa madogomadogo kama nguvu kazi ili waongeze uzalishaji ndani ya jeshi hilo.

Mkuu wa Jeshi la Magereza, Kamishna Jenerali, John Minja (kushoto) akimkabidhi Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati) taarifa ya kiutendaji ya Jeshi hilo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya. Viongozi hao wa Wizara walifanya ziara ya kikazi katika ofisi ya Makao Makuu ya jeshi hilo, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Post a Comment