Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar waliobomolewa nyumba zao zilizokuwa mabondeni wakiwa nje ya Mahakama Kuu ya Ardhi jijini Dar.
Baadhi yao wakionekana kutafakari ili kujua hatima ya kesi hiyo.
Wakazi wanaodaiwa kubomolewa nyumba zao za mabondeni wakiwa wamekaa nje ya Maduka yaliyopo karibu na eneo la mahakama hiyo.
KESI ya
kupinga bomoabomoa iliyofunguliwa na Mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia
(CUF) katika Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi jijini Dar es salaam
imeunguruma tena leo ambapo baadhi ya wakazi waliobomolewa nyumba
walionekana kukusanyika nje ya mahakama hiyo.
Kesi hiyo
namba 822 ya mwaka 2015 inasikilizwa na Jaji Penterine Kente huku
upande wa walalamikaji wakisimamiwa na wakili Abubakar Salim.
Kamera
yetu ya mtandao huu wa Gpl ilifika mahakamani hapo leo asubuhi na
kukuta wananchi hao wakiwa nje ya mahakama hiyo na ilikuwa bado
haijaanza kusikilizwa muda wa saa tano asubuhi. Wananchi hao
walijikusanya nje kama picha zinavyoonesha.
No comments:
Post a Comment