Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amesema kukosesha watu chakula
kutumika kama silaha katika mzozo wa Syria ni uhalifu wa kivita.
Ban Ki Moon amezituhumu pande zote nchini humo kukosa busara kutokana na hatua hiyo.
Ufaransa,
Uingereza na Marekani wametoa ombi la kufanyika kwa kikao cha dharura
cha Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, kutaka kuondolewa kwa hali
hiyo ya kuzingirwa, ambako maelfu ya watu wamekwama na pia kutaka,
misaada ifikishwe.
Kamishna
wa Shirika hilo la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa Zeid Ra'ad Al
Hussein amesema wote waliohusika na kuwakalisha watu njaa washtakiwe.BBC
No comments:
Post a Comment