Idadi ya Raia wa kigeni kutoka nchini Ethiopia waliokuwa wakisafirishwa na Gari la magazeti la kampuni ya Mwananchi Communication Ltd imefikia 12 baada ya wengine 4 kukamatwa Jioni wakiwa Eneo la Kibwabwa mjini Iringa wakiwa wamefichwa porini.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Iringa Peter Kakamba amesema kuwa tayari ametuma usafiri kwenda kuwabeba Raia hao ambao wanadai walishushwa katika gari hilo aina ya Hiace ili kuvuka eneo la ukaguzi wa Magari ( check pointi) kijiji cha Igumbilo nje kidogo ya mji wa Iringa.
Wakati huo huo Kampuni ya Mwananchi Communication Limited (MCL) imetoa ufafanuzi kuhusiana na kuhusishwa na kadhia hiyo. Soma zaidi:
No comments:
Post a Comment