Serikali Kuanzisha Vyuo vya vya Uvuvi Kuongeza Ujuzi kwa vijana - LEKULE

Breaking

28 Jan 2016

Serikali Kuanzisha Vyuo vya vya Uvuvi Kuongeza Ujuzi kwa vijana



Serikali imekusudia kuanzisha Vyuo vya Uvuvi katika maeneo yote yanayozungukwa na bahari ili kuwafundisha vijana mbinu sahihi za kufanya shughuli za Kilimo,Mifugo na Uvuvi ili kuwawezesha kukuza vipato vyao kwa kujiajiri.

Hayo yamesemwa leo Bungeni Mjini Dodoma  na Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe.William Tate  Ole Nasha akijibu swali la Mhe. Hamidu Hassan Bolali Mbunge wa Mchinga (CUF) kuhusu umuhimu wa kujenga chuo cha uvuvi mkoani Lindi ili kuwaongezea vijana ujuzi wa kazi hiyo.

Ameongeza kuwa wizara inatambua umuhimu wa kuwafundisha vijana mbinu sahihi za kufanya shughuli za uvuvi kilimo na ufugaji  na kwa sasa wizara kupitia Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvivu (Fisheries Education and Training Agency (FETA) imeanzisha Chuo cha Uvuvi Mikindani Mtwara kwa lengo la kusogeza huduma ya mafunzo ya uvuvi kwa wananchi hususani vijana walioko ukanda wa kusini mwa Tanzania ukiwamo mkoa wa Lindi.

Mhe.William Tate Ole Nasha amesema uanzishwaji wa Vyuo vya Uvuvi sio kwa maeneo yanayozungukwa na bahari ila kwa maeneo mengine pia ili kuwezesha vijana kupata ujuzi zaidi sio katika uvuvi pekee bali pia katika kilimo na ufugaji

Mbali na Chuo cha Uvuvi Mikindani  Mtwara pia kuna vyuo vingine kama vile Chuo cha Mbegani Mtwara  chenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 120 , Chuo cha Kibilizi Kigoma na  Chuo cha Nyegezi Mwanza.

Mbali za Vyuo hivyo serikali imehaidi kujenga vyuo Tanzania nzima ili kuwawezesha vijana  wengi zaidi kupata kupata ujuzi zaidi katika Kilimo, Uvuvi na Ufugaji ili kuendeleza ukuaji wa sekta hiyo na kuwezesha vijana kujiajiri wenyewe kupitia mafunzo wanayapata.

Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) itaanza kutoa mafunzo ya uvuvi katika Chuo cha Uvuvi Mikindani ya muda mfupi kwa mwaka 2016/2017 na yale ya Astashahada na Stashahada yataanza mwaka 20017/2018.

No comments: