Kundi moja la
wapiganaji wa jihad lililobuniwa miaka mitatu iliopita limekiri
kutekeleza mashambulio mawili ya hoteli katika eneo la Afrika Magharibi
katika kipindi cha miezi miwili.
Kundi hilo linalojiita
al-Murabitoun ,lina makao yake katika jangwa la Sahara kaskazini mwa
Mali na lina wapiganaji walio watiifu kwa mwanamgambo wa Algeria Mokhtar
Belmokhtar.Mnamo mwezi Novemba mwaka 2015,kundi hilo lilisema ndilo lililohusika na utekaji wa hoteli ya Radisson Blu Hotel katika mji mkuu wa Mali Bamako.
Taarifa ilioripotiwa na shirika la habari la Mauritania al-Akbar lilisema kuwa shambulio hilo lilitekelezwa kwa ushirikiano na kundi la al Qaeda katika eneo la Islamic Maghreb{AQIM}.
Mwezi Januari mwaka 2016,taarifa iliotolewa na AQIM ilisema kuwa al-Murabitoun ndio lililoktekeleza shambulio hilo katika hoteli ya Splendid katika mji mkuu wa Burkina Faso Ouagadougou.
Lakini aliondoka mwaka 2012 baada ya kukosana na viongozi wake.
Mda mchache baadaye, mnamo mwezi Januari mwaka 2013,alijipatia sifa mbaya ya kimataifa kwa kuagiza shambulio la kiwanda cha gesi cha Amenas nchini Algeria.
Wapiganaji chini ya uongozi wake waliwateka mateka kadhaa na kabla ya jeshi la Nigeria kudhibiti kiwanda hicho siku tatu baadaye, wafanyikazi 40 na wapiganaji 29 waliuawa.
No comments:
Post a Comment