Gabo Zigamba mwigizaji wa filamu
UNAPOSIKIA
jina la Gabo Zigamba si jina geni katika tasnia ya filamu , Gabo
amejizolea umaarufu katika tasnia ya filamu baada ya kufanya vizuri na
kuwachanganya wapenzi wa filamu Bongo, wengi wakiamini kuwa ni kijana wa
Kimachinga kutoka Kusini kumbe ni Mdigo na Mhehe.
Jina
halisi la msanii huyu ni Salim Ahmed Issa akisema hilo ni jina la
kliniki, lakini jina la riziki anajulikana kama Gabo Zigamba, amezaliwa
Mitaa ya Mshindo na kukulia katika mitaa ya Kitanzini kama ingekuwa hapa
Dar ni mtoto aliyezaliwa Ilala na kukulia mitaa ya Kariakoo akilelewa
na mama yake Rafia Issa Kiyeyeu.
Babu yake
ni Mtogapaafwe Kiyeyeu familia ya Martin Kiyeyeu mtu maarufu sana
Iringa ambaye kila unapotaja jina lake wengi ukumbuka kuhusu maajabu ya
kaburi lake, Gabo anasema kuwa ameishii pande zote mbili lakini sehemu
kubwa sana ni Iringa kwa mama yake akisoma Ipogolo Iringa.
Gabo anasema yeye ni mwanaharakati sauti ya wanyonge isiyosikika hivyo alianza harakati zake kitambo akifiria ni jinsi anavyoweza
kufikisha ujumbe kwa jamii husika kwa kupitia sanaa na hasa filamu,
wengi wanaamini kuwa sinema yake ya kwanza ni Bado Natafuta lakini ni
kazi ilifanya vizuri baada ya kupewa nafasi.
SANAA ALIANZA LINI
Gabo kuigiza alianza kitambo lakini rasmi ilikuwa ni 2006 kwa kushiriki katika vikundi mbalimbali huku akiwa na shauku kubwa ya kuwa nyota na kufikia lengo lake la kuwatetea wasio na nafasi anasema haikuwa rahisi sana kwani kulikuwa na changamoto nyingi ambazo hazikumkatisha tamaa.
Harakati
zangu hazikuja kama upepo sinema yangu ya kwanza ilikuwa ni Olopong
iliyotengenezwa na Al Riyamy Production chini ya Khalfan Abdalah, hapo
milango ndio ilifunguka kwani baada ya hapo nikacheza 007 Boyz,”anasema
Gabo.
Baada
hapo alishiriki katika filamu ya The Plan, na kujiunga na kampuni ya
marehemu Juma Kilowoka ‘Sajuki’ Wajey Film akishiriki katika sinema zao
kama mwigizaji na kufanikiwa kucheza filamu Mchanga na Keni, The killer
na 007 Days alikuwepo hapo akijifunza vitu katika tasnia ya filamu.
No comments:
Post a Comment