1. Ukawa waikamata Dar es Salaam..
Kwa
vyovyote vile hii ni habari kubwa inayopewa nafasi ya kwanza na mtandao
wa mjengwablog.com. Tumepata kuchambua, kuwa umeya Dar unapaswa
kuangaliwa katika picha kubwa. Ifahamike, Dar ni 'mkoa wa kitaifa' na
kuwa meya Dar ni nafasi kubwa sana kitaifa. Si ajabu, kuwa vita haikuwa
ndogo, baina ya upinzani na chama tawala, katika Hii ni vita ya
kuipigania Dar.
CCM kupoteza nafasi za umeya kwa Ilala na Kinondoni kwaweza kutatafsiriwa kama kupoteza nguvu zake za kisiasa ndani ya jiji kitovu cha siasa na biashara hapa nchini. Ingawa, matokeo hayo yanaweza pia kuipa nafasi CCM kuonyesha uwezo wake wa kuendesha siasa za upinzani dhidi ya halmashauri zenye kuongozwa na vyama pinzani. Kuonyesha mbadala wakiwa nje.

Naam,
demokrasia imechukua mkondo wake, ni wakati sasa wa waliochaguliwa
kuendesha halmshauri kufanya kazi ya kuwatumikia wananchi kwa
kushirikiana na Serikali Kuu iliyo madarakani.
Na katika
kuimarisha ubora wa uwakilishi wa watu, kama tulivyopendekeza juma moja
lililopita, kuwa huko tuendapo ungekuwepo utaratibu wa meya kuchaguliwa
na wakazi wenyewe kwa kupigiwa kura, na si kundi dogo la
madiwani.Ndivyo wafanyavyo wenzetu walioendelea.
2. TCRA kuvifungua vituo 6 vya TV na redio 20
Hii ni
habari inayochukua nafasi ya pili kwa mujibu wa mtandao
waMjengwablog.com. TV na redio ni vyombo vyenye kuhusu jamii pana katika
kupata habari na hata burudani. Inaripotiwa kuwa wahusika hawajalipa
ada wanazopaswa kulipa. Imeandikwa pia, kuwa ifikapo kesho saa sita,
kama hawajalipa, vituo vyao vitafungwa. Na baadhi ya wahusika
wameonyesha kutofautiana na TCRA, ni kupitia kwenye magazeti, si redio
wala tv, iwe za kwao au za washindani wao wengine kibiashara!
3. Polisi yawasaka wahariri Mawio
Ni habari itakayowavuta wasomaji wengi. Nasi mtandao wamjengwablog.com tunaipa nafasi ya tatu kwa ukubwa.
No comments:
Post a Comment