FIFA imezifungia Real Madrid na Atletico Madrid, hii ndio mipango ya Ronaldo itakayokwama - LEKULE

Breaking

15 Jan 2016

FIFA imezifungia Real Madrid na Atletico Madrid, hii ndio mipango ya Ronaldo itakayokwama

Vilabu vya Real Madrid na Atletico Madrid vya jiji la Madrid Hispania, January 14 shirikisho la soka ulimwenguni FIFA limetangaza adhabu ya kuvifungia vilabu hivyo, kutokana na kukiuka sheria ya usajili ya wachezaji waliochini ya umri wa miaka 18. Adhabu hiyo waliyopewa Real na Atletico waliwahi pia kukumbana nayo FC Barcelona.
January 14 FIFA imetangaza kuvifungia vilabu hivyo kutosajili katika vipindi viwili vijavyo vya usajili, kutokana na kukiuka sheria ya usajili kwa wachezaji waliochini ya umri wa miaka 18, adhabu ya Real Madrid na Atletico Madrid itamalizika mwaka 2017, lakini adhabu hiyo imekwenda pamoja na faini ya pound 620,000 kwa Atletico na pound 250,000 kwa Real.
Real Madrid's Portuguese forward Cristiano Ronaldo (R) kicks the ball past Atletico Madrid's Uruguayan defender Diego Godin (L) during the Spanish league football match Club Atletico de Madrid vs Real Madrid CF at the Vicente Calderon stadium in Madrid on October 4, 2015. AFP PHOTO/ PIERRE-PHILIPPE MARCOU (Photo credit should read PIERRE-PHILIPPE MARCOU/AFP/Getty Images)
Sheria ya usajili ya FIFA kwa wachezaji waliochini ya umri wa miaka 18, inataka mchezaji ili aweze kusajiliwa kutoka nchi moja kwenda nyingine, moja kati ya vigezo vya sheria hiyo ili mchezaji aweze kusajiliwa kutoka nchi moja kwenda nyingine, hadi wazazi wake wawe wanahama kutoka nchi hiyo kwenda nchi atakayosajiliwa na sio kwa sababu za kimpira au vipi labda wazazi wanahamia nchi hiyo kikazi.
Kufuatia adhabu hiyo ya kutosajili kwa vipindi viwili vya usajili inatajwa huenda ikaathiri mipango ya Cristiano Ronaldo anayehusishwa kutaka kuihama klabu hiyo kwa siku za karibuni hasa wakati wa dirisha la usajili la mwezi August 2016, kwani Real Madridhaitoruhusu mchezaji yoyote kuhama kwa sababu haiwezi kufanya usajili.

No comments: