Wahamiaji
waliozuiliwa na vikosi vya usalama vya Hungary baada ya kuvuka uzio wa
nyaya za chuma uliojengwa kwenye mpaka kati ya Serbia na Hungary,
Jumanne 15 Septemba 2015.
Na RFI
Umoja wa
Ulaya hauna "zaidi ya miezi miwili" ili kudhibiti mgogoro wa uhamiaji au
utapata athari katika eneo la Schengen kwa uhuru wa kutembea kwa watu
na mzunguko wa vitu, amesema Jumanne hii rais wa Baraza la Ulaya, Donald
Tusk mbele ya Bunge la Ulaya.
"Baraza
la mwezi Machi liitakuwa fursa ya mwisho ili kuona kama mkakati wetu
unafanya kazi. La sivyo, tutakabiliana na matokeo mabaya kama vile
kuanguka kwa Schengen", Donald Tusk amesema.
Donald
Tusk pia ameonya dhidi ya hatari ya kushindwa kwa "mradi wa kisiasa" wa
Umoja wa Ulaya kama jamii nzima itashindwa kudhibiti ukaguzi wa mipaka
yake ya nje.
Ulaya inakabiliwa tangu mwaka jana na mgogoro mbaya wa uhamiaji. Mgogoro kama huo ulitokea mwishoni mwa Vita vikuu vya pili.
Rais wa
Tume ya Ulaya, Jean-Claude Juncker, ametoa kauli pia ya tahadhari,
akizitolea wito nchi wanachama kutekeleza mikakati iliyopendekezwa na
mkutano wao wa pamoja: kuundwa kwa kikosi cha walinzi wa mipaka ya
Ulaya, vituo vya ukaguzi au "hot spots" katika mipaka ya nje na kutambua
maeneo wanakoishi wakimbizi katika nchi wanachama.
Hungary, Slovenia, Austria, Denmark na Sweden tayari wameanzisha utaratibu wa ukaguzi kwenye mipaka.
"Mipaka ya pamoja, usimamizi wa pamoja. Kama hatutatekeleza hilo, Schengen haina muda mrefu wa kuishi", Donald Tusk amesema.
"Tume ya
Ulaya tayari iliwasilishwa mambo yote yanayohitajika ili kusimamia
mgogoro wa wakimbizi", Tusk amebaini, huku akitoa wito kwa nchi
wanachama kutekeleza mambo hayo tangu sasa na kupata "mafanikio ya
ujenzi wa Ulaya"
No comments:
Post a Comment