Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (kulia), akizungumza katika
mkutano na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Taasisi ya Moyo ya
Jakaya Kikwete Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dar es Salaam leo asubuhi
wakati akitoa mwito kwa wananchi hasa wa Wilaya ya Kinondoni na maeneo
mengine ya jiji la Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kupimwa maradhi ya
moyo bure katiza zoezi litakalofanywa na madaktari kutoka taasisi hiyo
litakalofanyika viwanja vya leaders kesho kutwa January 23, 2015.
Kushoto ni Meneja wa Taasisi hiyo, Salome Kassanga na Kaimu Mkurugenzi
wa Taasisi hiyo, Profesa Mohamed Janabi.
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Profesa Mohamed Janabi (kushoto),
akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,
Paul Makonda.
Meneja
wa Taasisi hiyo, Salome Kassanga (kushoto), akimuelekeza jambo DC
Makonda. Katikati ni Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Moyo wa Taasisi hiyo,
Dk.Peter Kisenge.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.
MKUU
wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda kesho kutwa anatarajia kuongoza
wananchi wa wilaya yake na wakazi wengine wa jiji la Dar es Salaam
katika upimaji wa magonjwa ya moyo utakaofanywa bure na madaktari kutoka
Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), katika viwanja vya Leaders
Club.
Upimaji huo utatoa fursa ya kubaini wagonjwa wa wilaya hiyo kwa kuwa wananchi wengi hawajui magonjwa ya moyo yanaweza pia kusababishwa na shinikizo la damu na ni chanzo kikubwa cha magonjwa ya macho,upungufu wa nguvu za kiume, kiharusi, figo na kutokuzaa.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam leo asubuhi, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo
Profesa Mohamed Janabi alisema kutokana na umuhimu wa wananchi kujua
afya zao na kupatiwa matibabu mapema kesho wataungana na Makonda katika
kuwapatia vipimo wakazi wa kinondoni.
Alisema
ugonjwa wa moyo ni hatari na asilimia kubwa ya wagonjwa hao wanatembea
na kufanya kazi zao kwakuwa ugonjwa huo hauna dalili hivyo haja ya kila
mmoja kupima na kujua afya yake ni muhimu.
“Pia
wengi wanaougua shinikizo la damu hawajua wanaweza kuwa na magonjwa ya
moyo na kujikuta wakisababisha kuua figo,macho,nguvu za kiume,kuugua
kiharusi na kukosa watoto upimaji huu ni hatua nzuri kwa wananchi wa
kinondoni hivyo tumeridhia kuwapima na kuwapatia matibabu bure,”alisema.
Alisema
taasisi hiyo itakuwa kamili katika kila sekta kesho kutwa viwanja vya
Leaders Club ili wananchi wenye magonjwa yanayoshabihiana na moyo waweze
kupewa tiba katika hospitali za wilaya hiyo ikiwemo Mwananyamala na
wale walioathirika na ugonjwa wa moyo waweze kutibiwa Hospitali ya Taifa
ya Muhimbili.
Profesa
Janabi alisema pia watahakikisha madaktari wa ushauri wanatoa elimu
ipasavyo juu ya kuepuka ugonjwa wa moyo na shinikizo la damu ambao hauna
tiba na jinsi ya kuzingatia lishe.
“Ni
muhimu kujua ongezeko la matumizi ya vyakula vya wanga kwa wingi pia ni
hatari katika kuongeza uzito hivyo kusababisha shinikizo la
damu,”alisema
Kwa
upande wake Makonda aliwataka wananchi kuelewa kuwa ugonjwa wa moyo ni
hatari na matibabu yake ni gharama hasa kwa wale wanaosafirishwa nje ya
nchi hivyo ni vyema kuitumia fursa hiyo kesho.
Alisema
serikali imeona haja ya kuboresha afya za wananchi ili kukuza uchumi na
hatua hiyo ya kusaidia upimaji wa bure itapunguza hatari ya ugonjwa huo
kwa watu wengi wanaopoteza maisha kila siku.
No comments:
Post a Comment