Bomu
lililotegwa ndani ya gari limelipuka nje ya mgahawa mmoja uliopo katika
ufukwe wa bahari katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu,kulingana na
maafisa wa polisi.
Walioshuhudia
wamemwelezea mwandishi wa BBC Ibrahim Aden kwamba gari hilo lililojaa
vilipuzi liligonga mgahawa huo maarufu wa Lido Beach kabla ya watu
watano kujitokeza na kuanza kufyatua risasi.
Haijulikani iwapo kumekuwa na majeruhi.
Hakuna
kundi lililokiri kutekeleza shambulizi hilo,lakini kundi la Alshabaab
ndilo linaloshukiwa kwa kutekeleza mashambulizi mengine kama hayo hapo
awali.
Ufukwe wa bahari nchini Somalia
Mgahawa wa Lido Beach uliopo pembezoni mwa Mogadishu,huwavutia maelfu ya vijana wa Somalia wanaojifurahisha.
Migahawa kadhaa imefunguliwa katika ufukwe huo katika miaka ya hivi karibuni.
Afisa
mkuu wa polisi katika eneo hilo Meja Abdiqadir Ali amekiambia chombo cha
habari cha reuters kwamba shambulio hilo lilitokea katika lango la
mgahawa huo.
Amesema kuwa uchunguzi unaendelea
No comments:
Post a Comment