BODABODA JIJINI ARUSHA NA UTATA ULIPO NA WAENDESHA PIKIPIKI ZA KAWAIDA. - LEKULE

Breaking

27 Jan 2016

BODABODA JIJINI ARUSHA NA UTATA ULIPO NA WAENDESHA PIKIPIKI ZA KAWAIDA.


 Waendesha pikipiki wakiwa mbele ya ofisi ya Mkuu wa mkoa.

Na Vero Ignatus , Arusha.

Chama cha waendesha bodaboda Jijini Arusha ( UWAPA) chaiomba serikali kutatatua utata uliopo kati ya waendesha bodaboda na waendesha pikipiki za kawaida kwa kuwawekea alama maalumu ambayo itawatambulisha, hii ni kutokana na maandamano ambayo yamefanyika siku ya tar 25./1 /2016 kwani ni kinyume kwakuwa chama hakina taarifa yeyote kuhusu maandamano hayo.
Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa UWAPA bwana Godlight Rugemalila ambapo amesema ametoa taarifa polisi kutokana na maandamano hayo na amesema jambo walilolifanya siyo sahihi kwa hao walioratibu maandamano hayo ,na amewataka waendesha bodaboda wote kama kuna jambo lolote watalipata ofisini wafuate utaratibu wasikurupuke
 Amesema kuwa yapo makundi ya aina mbili kwa waendesha bodaboda,kundi la kwanza ni walimesajiliwa na UWAPA hawana vituo maalum , kundi la pili ni waendesha pikipiki za kawaida hawa hawajasajiliwa na idadi yao ni kubwa ambao huwaharibia wale ambao wanafanya biashara halali ya kubeba abiria
Amesema kuwa wao kama UWAPA hawajapanga maandamano walipata taarifa kutoka kwa watu binafsi na walishtushwa kusikia kuna maandamano hayo na ameongeza kuwa wanaendelea kufanya utafiti kwa kushirikiana na jeshi la polisi ili kufahamu ni wakina nani wanahusika kuratibu maandamano hayo . 
Amewataka waendesha bodaboda wafuate sheria za usalama barabarani kama zinavyoelekeza, wawe na leseni, wavae kofia ngumu ,wapaki kwenye vituo vilivyosajiliwa ,amewashauri abiria wanaotumia usafiri huo wachukue bodaboda zilizopo kwenye vituo kwani akipata tatizo lolote ni rahisi yeye kusaidika tofauti na akichukua pikipiki ambayo ameiona barabarani inapita utakosa pa kupeleke malalamiko yako maana kila kituo kina kiongozi.
Ameainisha waendesha bodaboda waliosajiliwa na wanaotambulika hadi sasa jumla yao ni 2950 ,vituo vilivyosajiliwa 144 na vituo bubu ambavyo bado na vinatazamia kupata usajili ni 55 hivyo amewataka waendesha pikipiki wote wajisajili kwenye chama hii ni kwa faida yao maana watatambulika watasaidika mara wapatapo tatizo na hii itawaepusha kuingia kwenye lawama za mara kwa mara kuwa waendesha pikipiki ni wakwapuaji na wanatumika kwenye matukio ya uhalifu.
 Amehitimisha kwa kusema kuwa UWAPA ni umoja wa wawaendesha bodaboda jijini Arusha na umoja huu ulisajiliwa marchi 2012 na unatambulika kiserikali,lengo ni kuwaleta pamoja waendesha bodaboda na huwa wanapatiwa mafunzo na RTO chini ya kitengo cha usalama barabarani , hivyo amewataka wananchi wafahamu kuwa wapo waendesha bodaboda hawa wanapaki maeneo yaliyoidhinishwa na ni vituo halali na waendesha pikipiki ni yeyeote yule unayeweza mchukua barabarani hana kituo.
Maandamano hayo yalifanyika kuelekea kwa mkuu wa mkoa wa Arusha wakiwa na madai ya wakimtaka mkuu huyo wa mkoa atoe tamko kuhusu kusumbuliwa kwao na askari wa usalama barabarani .(P.T)

No comments: