Baada ya kutolewa Mapinduzi Cup, Simba yafanikiwa kulipiza kisasi kwa Mtibwa Sugar. - LEKULE

Breaking

16 Jan 2016

Baada ya kutolewa Mapinduzi Cup, Simba yafanikiwa kulipiza kisasi kwa Mtibwa Sugar.



Baada ya wekundu wa msimbazi Simba kutolewa katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi na Mtibwa Sugar ya Manungu Morogoro. January 16 katika mchezo wa Ligi Kuu walikutana tena, hiyo ilikuwa ni nafasi kwa Simba kulipa kisasi kwa Mtibwa Sugar au kuendeleza rekodi ya kupokea vipigo.
Simba ambayo ilikuwa inacheza mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu toka ianze kufundishwa na kocha wake msaidizi Jackson Mayanja, ambaye kwa sasa anasimama kama kocha mkuu baada ya Simba kumfukuza kocha wake wa kiingereza Dylan Kerrsiku kadhaa nyuma, Simba kupitia kwa  mshambuliaji wake wa kimataifa wa UgandaHamisi Kiiza, walifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0.

Goli la Simba lilifungwa na Hamisi Kiiza dakika ya 8 kipindi cha kwanza, goli hilo lilionekana kuwagawanya Mtibwa Sugar kwa kipindi cha kwanza, kwani Simba kwa kiasi kikubwa waliutawala mchezo, Mtibwa walijaribu kutafuta goli la kusawazisha kwa bidii kipindi cha pili, jitihada ambazo hazikuzaa matunda.
Matokeo ya mechi nyingine zilizochezwa January 16
  • JKT Ruvu 1 – 5 Mgambo JKT
  • Toto Africans 0-1 Tanzania Prisons
  • Stand United 1-0 Kagera Sugar
  • Mbeya City 1-0 Mwadui FC
  • Coastal Union 1-1 Maji Maji FC

No comments: