SKOFU Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo jududi
za madaktari na huduma zinazotolewa katika Tasisi ya Moyo ya Jakaya
Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Mhimbili.
Amepongeza
leo wakati akizungumza na waandishi wa habari Askofu Pengo pia amesema
yeye alikua anaogopa kutokana na taarifa zinazotolewa kwenye vyombo vya
habari juu ya Oparesheni tata iliyowahi kufanyika katika hospitali ya
Taifa ya Mhimbili.
Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo alilazwa katika taasisi ya moyo tangu Januari Mosi.
Kwa
upande wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na Wazee,
Ummy Mwalimu amesema kuwa Serikali imeokoa kiasi cha hilingi bilioni
nne ambazo zilikua zipotee kwaajili ya kupeleka wagonjwa wa moyo kwenda
kutibiwa nje ya nchi.
Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo akingia
katika ukumbi wa mikutano katika kitengo cha Moyo cha Taasisi ya Jakaya
Mrisho Kikwete kilichopo katika Hospitali ya Taifa ya Mhimbili.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na Wazee, Ummy Mwalimu akimkaribishaAskofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo ili aweze kuzungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo na kuwapongeza jopo la
Madaktari waliomhudumia katika Hospitali ya Mhimbili.
Kulia
ni aliyekuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwashamu
Askofu Titus Mdoe na Askofu Mkuu wa Jimbo la Songea, Damian Dallu wakiwa
katika mkutano wa Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwadhama
Polycarp Kardinali Pengo na waandishi wa habari katika ukumbi wa Mkutano
wa Kitengo cha Moyo cha Jakaya Mrisho Kikwete iliyopo katika Hospitali
ya Taifa ya Mhimbili.
Askofu
Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na Wazee, Ummy
Mwalimu na Kushoto ni Askofu Mkuu wa Jimbo la Songea, Damian Dallu.
Katika
mkutano huo Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwadhama
Polycarp Kardinali Pengo alitoa zawadi za kadi za pongezi kwa baadhi ya
madaktari mara baada ya kuzungumza na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam leo.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na Wazee, Ummy Mwalimu
akiteta jambo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya
Mrisho Kikwete iliyopo katika hospitali ya Taifa ya Mhimbili, Profesa
Mohamed Janabi.
Katibu
Mkuu wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na Wazee
Mpoki Ulisobisya akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusiana
na swali lililoulizwa na mwandhishi wa habari kuwa Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na Wazee haitoi ruhusa ya mtu yoyote
kwenda kutibiwa nje ya nchi na ruhusa hiyo hutolewa na Madaktari wenyewe
ambao walikua wanamtibia mgonjwa.
No comments:
Post a Comment