Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, imekemea tabia ya kuadhibu wanyama kwenye maeneo ya migogoro baina ya wakulima na wafugaji.
Hayo
yalisemwa jana na Mkurugenzi wa Huduma za mifungo Tanzania katika
wizara ya Kilimo, mifugo na Uvuvi, Dkt. Abdu Hayghaimo wakati
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Hayghaimo
alisema kuwa wananchi wenye tabia ya kuwadhuru wanyama waiache mara
moja kwa kuwa wanyama hao wanaongozwa na binadamu kwenye maeneo
yasiyowahusu wanayama.
Alisema
kuwa kwa mujibu wa sheria ya ustawi wa wanyama wanahaki ya chakula,
maji, mahali pazuri pakupumzika, kulindwa dhidi ya maumivu yeyote,
magonjwa na mateso ikiwa pamoja na kuwasaabishia kifo.
Pia
wizara imewatahadharisha wananchi wote wanaochukua sheria mkononi na
kusababisha madhara makubwa yasiyokubalika kutokana na migogoro ya
migogoro ya wakulima na wafugaji kuwa huwanyima wanyama haki zao ni
uvunjifu wa amani.
Jamii
imeshauriwa kuwa itafute suruhu ya migogoro hiyo kupitia kamati
zitakazo matumizi endelevuya ardhi kwa mujibu wa walaka unaoandaliwa na
wizara.
No comments:
Post a Comment