WAZIRI
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ameuagiza uongozi wa mkoa
wa Kagera,Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (Takukuru) na vyombo
vya dola, kuwashughulikia wala rushwa katika mradi ya umeme vijijini.
Amezitaka
taasisi hizo na uongozi huo, kuchunguza na kuwabaini wanaojihusisha na
vitendo hivyo katika mradi huo, unaosimamiwa na Wakala wa Umeme Vijijini
(REA), ili wawachukulie hatua ikiwamo kuwafikisha mahakamani.
Alitoa
kauli hiyo jana baada ya kupata malalamiko kutoka kwa wananchi na
madiwani wanne wa Halmashauri ya wilaya ya Karagwe , wakiongozwa na
Mbunge wao, Innocent Bashungwa, ambapo walisema wafanyakazi wa kampuni
hiyo wamekuwa wakitoa umeme kwa watu wanaowapatia fedha za pembeni na
kusababisha hata ramani ya ufungaji umeme kutofuatwa.
Walisema
kwa nyakati tofauti kuwa watu wanaojitambulisha kuwa wanafunga umeme
vijijni, wamekuwa wakiwataka wananchi watoe chochote kuanzia Sh 75,000
na kuendelea wakati wameishalipia Sh 27,000 zinazotakiwa kupata huduma
hiyo.
Mkuu
wa Mkoa wa Kagera, John Mongella alisema amejaribu kufanya utafiti na
kugundua kuwa hali hiyo imekuwa ikisababishwa na usimamizi hafifu wa
kampuni inayosimamia mradi wa REA.
Wakati
huohuo Waziri Muhongo ametaka uongozi wa Shirika la Umeme (Tanesco)
mkoa na wilaya ya Karagwe na mkandarasi anayehusika na mradi wa REA,
kujibu tuhuma hizo kama wameshazisikia na wamezitatua vipi.
Mhandisi
Mshauri wa kampuni ya Urbanand Rural inayoshughulikia ufungaji umeme wa
REA eneo hilo, Julius Kateti , alithibitisha kuwepo kwa udanganyifu
unaofanywa na baadhi ya wafanyakazi wake wasio waaminifu.
Alisema kutokana na hilo, mpaka sasa ameshawafukuza kazi zaidi ya wafanyakazi 100 kati ya 680 huku kesi nane zikiwa Polisi.
Baada ya jibu hilo, Muhongo alisema kuwa tatizo hilo limeonekana ni la mkoa mzima na ndipo aliagiza Mkurugenzi wa Usambazaji wa Umeme nchini kutoka REA makao makuu, kufika mkoani Kagera mara moja ili kukaa na uongozi wa Tanesco na wa mkoa wa Kagera kuhakikisha wanatatua masuala hayo.
Baada ya jibu hilo, Muhongo alisema kuwa tatizo hilo limeonekana ni la mkoa mzima na ndipo aliagiza Mkurugenzi wa Usambazaji wa Umeme nchini kutoka REA makao makuu, kufika mkoani Kagera mara moja ili kukaa na uongozi wa Tanesco na wa mkoa wa Kagera kuhakikisha wanatatua masuala hayo.
Meneja
wa Tanesco Kanda ya Ziwa, Amos Maganga alimweleza mkandarasi wa REA
kuwa ikibainika alichepusha mradi na kupeleka nje ya kilometa 453 za
awamu hii kinyume cha mkataba, Tanesco haitatoa fedha ya Serikali
kulipia ukiukwaji huo, bali mkandarasi atawajibika mwenyewe.
Akifafanua
hilo, Profesa Muhongo alisema serikali imeweka azimio kuwa kampuni
itakayobainika kunyanyasa wananchi, haipaswi kupata kazi tena katika
awamu zijazo, kwani Watanzania wamechoka na ahadi zisizotekelezeka.
No comments:
Post a Comment