Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Willium Lukuvi akizungumza na
wakuu Idara katika wizara ya Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi
alipokutana nao leo alipokaribishwa kwa mara ya kwanza katika wizara
hiyo, tangu achaguliwe na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt
John Pombe Magufuli kuwa Waziri wa wizara, na kuwaagiza wakuu wa idara
katika wizara hiyo kutoa taaarifa za idara zao ifikapo jumatatu ya wiki
ijayo.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Willium Lukuvi akipokea ripoti
ya wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Katibu mkuu wa
wizara yaWizara wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Alphayo Kidata.
Kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
Angelina Mabula.
Naibu
Waziri wa Wizara Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula
akipokea ripoti ya wizara ya Ardhi, nyumba na Maendeleo makazi leo
walipokutana na wakuu wa idara mbalimbali leo jijini Dar es Salaam.
katikati ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Willium Lukuvi.
Naibu
Waziri wa Wizara Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula
akizungumza na wakuu wa Idara wa wizara hiyo leo jijini Dar es Salaam,
akizungumzia kuhusiana na wawekezaji ambao watakua hawajaendeleza ardhi
ambayo walichukua kwa aajili ya uwekezaji na ardhi hiyo kurudishwa kwa
wananchi. Kutoka Kulia ni Katibu Mkuu wa wizara ya Ardhi Nymba na
Maendeleo ya Makazi, Alphayo Midata, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Willium Lukuvi na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Ardhi, Nymba na Maendeleo ya Makazi, Selassie Mayunga.
Baadhi
ya waandishi wa habari pamoja na wakuu wa Idara za wizara ya Ardhi
Nyumba na maendeleo ya makazi leo jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment