Waziri
wa Habari, Utamaduni Wasanii na Michezo Nape Nnauye, amekanusha taarifa
iliyosambaa mitandaoni inayohusu wizara yake kukataza baadhi ya mavazi
hasa sehemu za mikusanyiko ya umma.
Amesema Taarifa hizo ni za uzushi na uongo, na kuwataka mamlaka husika kuwachukulia hatua watu waliotoa taarifa za uongo.
“Hizo
taarifa ni uzushi mtupu na uongo, mamlaka husika wachukue hatua,
watimize wajibu wao, watumie sheria iliyopo kuwachukulia hatua”, amesema Mh. Nape Nnauye.
Mwishoni
mwa wiki hii kuna taarifa ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii
ikionyesha ni taarifa kwa vyombo habari juu ya katazo la mavazi
yasiyofaa kwenye mikusanyiko ya watu, hususan hospitali, maofisini,
sokoni, na vyuoni
No comments:
Post a Comment