Naibu
Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medadi Kalemani (wa kwanza kulia)
akitoa maagizo ya kukamilika kwa mradi huo ifikapo february mwakani kwa
Mkurugenzi Mwandamizi wa Miradi TANESCO Bw.Gregory Chegere (wa kwanza
kushoto) alipofanya ziara yake leo katika mradi wa Tanzania Energy
Development Access Program (TEDAP) eneo la Mbagala Rangi Tatu,jijini Dar
es Salaam,Mradi huo utasaidia kusambaza umeme wenye nguvu ya kutosha na
unaotarajia kunufaisha zaidi ya wananchi elfu kumi wa eneo hilo,watatu
kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Paul
Masanja.
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medadi Kalemani (kushoto) akitoa
maagizo kwa Mkandarasi wa Kampuni ya SAE Power Lines Bw.Tahir Mehmood
(wa kulia) anayejenga mradi wa TEDAP eneo la Kurasini jijini Dar es
salaam kuhakikisha mpaka mwanzoni mwa mwakani awe amshafunga Transifoma
katika eneo hilo la mradi ni baada ya kutoridhishwa na kasi ya
utekelezaji wake katika mradi huo.
Mhandisi
Mkuu wa Miradi TANESCO Bw. Frank Mashalo (wa kwanza kulia) akimweleza
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medadi Kalemani (wa pili
kushoto)kuhusu maendeleo ya mradi TEDAP uliyopo maeneo ya Gongo la
Mboto jijini Dar es Salaam na (wa kwanza kushoto) ni Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Paul Masanja.
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medadi Kalemani (kushoto) akisikiliza
malalamiko ya mmoja wa wateja wa huduma za TANESCO Bw.Michael Sedyan,
Mkazi wa Sinza,hii ni baada ya Naibu waziri kufanya ziara ya kushtukiza
katika ofisi za Tanesco Magomeni leo jijini Dar es Salaam.
Afisa
Muendesha Mitambo kituo cha TANESCO Kipawa Bibi Zuhura Mmanyi (wa kwanza
kulia)akimweleza Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medadi Kalemani
(wa kwanza kushoto) namna mitambo ya eneo hilo inavyofanya kazi na
maeneo mitambo hiyo inayosambaza umeme ikiwemo eneo la Gongo la
mboto,Kiwalani,Segerea,Chang’ombe na Buguruni leo jijiji Dar es Salaam
Naibu waziri alipo fanya ziara yake katika ofisi hiyo (wapili kushoto ni
Mkurugenzi Mwandamizi wa Miradi TANESCO Bw.Gregory Chegere na wapili
kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Paul
Masanja.
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medadi Kalemani (wa kwanza kushoto)
akitoa maagizo kwa Mkandarasi wa Kampuni ya SAE Power Lines Bw.Stephen
Joseph (wa kwanza kulia) anayejenga Mradi wa TEDAP eneo la Gongo la
Mboto kuhakikisha umeme unaanza kuwaka katika mitambo hiyo ifikapo
mwishoni mwa mwezi Desemba 2015 kwa kuwa kila kitu kimeshakamilika
katika mradi huo na malipo yake tayari ameshamaliziwa kulipwa, (wapili
kushoto) ni Mkurugenzi Mwandamizi wa Miradi TANESCO Bw.Gregory Chegere.
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medadi Kalemani (kulia) akimsikiliza
mmoja wa wateja wa Ofisi ya TANESCO Magomeni Bw.Mohamed Bago Mkazi wa
Manzese alipokuwa akitoa kero yake kuhusu kusubiri zaidi ya masaa matatu
kupatiwa huduma ya tatizo ya luku yake ambayo haiingizi umeme,hiyo ni
baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika ofisi za Tanesco Magomeni.
No comments:
Post a Comment